​UTEUZI WA KIMUNGU | World Challenge

​UTEUZI WA KIMUNGU

Gary WilkersonMarch 11, 2019

"Mthiopiya, towashi ... alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, akawa akirejea, ameketi katika gari lake, na alikuwa akisoma nabii Isaya. Roho akamwambia Filipo, "Sogea karibu na gari hili" (Matendo 8:27-29).

Mtiopiya huyo, ambaye alikuwa mwekahazina wa Kandake, malkia wa Ethiopiya, alikuwa akienda hekalu huko Yerusalemu kuabudu, akiangalia kuingia katika njia mpya ya kuishi. Kupitia njia yote aliendelea kutafuta, na alikuwa akiketi karibu na barabara, akiisoma Maandiko katika mkokote wake.

Bwana alimwambia Filipo kusafiri kwenye barabara hii ili apate kukutana na Mthiopiya huu . Alimtii Bwana na alipomwona Mthiopiya akaenda kuzungumza naye, alimwona yule mtu akisoma kutoka Isaya 53:7: "Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, na kama vile kondoo anyamanzavyo mbele yao wakatao manyoya yake; naam, hakufungua kinywa chake."

Mtu huyo akamwuliza Filipo nini Maandiko yanamaanisha, na Filipo, akatambua kwamba moyo wa mtu huyo alikuwa na hamu kuhusu ukweli, ilianzia kwa ufafanuzi kamili wa ukweli wa Yesu Kristo. "Filipo akafungua kinywa chake, naye, akianzia kwa Andiko lilo hilo akamwambia habari njema juu ya Yesu" (8:35).

Sehemu ya Maandiko Mthiopiya alikuwa akiisoma kutoka katika Agano la Kale akisema kuhusu utimilifu wa unabii wa Yesu Kristo. Filipo alikuwa na uwezo wa kueleza juu ya mpango wa Mungu wa wokovu, ubatizo, ufalme mpya katika Mungu - yote hayo alikuwa ni kimali, kutimizwa kamili katika Mtu mmoja - Yesu. Mthiopiya alifungua moyo wake na akajibu ujumbe na akapokea uzima wa milele.

Wakati mwaminifu wakweli akizungumza Injili kwa moyo wa kupenda, miujiza hufanyika. Bado unaweza kuwa kwenye utafutaji wa kuelewa zaidi kuhusu Yesu. Ikiwa ndivyo, hakika Mungu atajibu kilio cha moyo wako kujifunza zaidi juu yake na kuleta mtu kwako. Au labda Bwana ataweka uhusiano wa Mungu ambapo utakuwa na uwezo wa kumuongoza mtu mwingine.

Download PDF