ASILI YA MUSAMAHA WA MUNGU | World Challenge

ASILI YA MUSAMAHA WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)August 9, 2018

Wakati mwingine Daudi aliteseka sana chini ya fimbo ya adhabu ya Bwana. Aliogopa kwamba Bwana amemchaa kabisa kwa sababu ya dhambi yake, wazo ambalo hakuweza kuvumilia, naye akamwombea Bwana, "Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu" (Zaburi 69:15). Alikuwa akisema, "Bwana, tafadhali usiniache niende mbali sana siwezi kwenda nje!"

Katika kukata tamaa kwa Daudi, maombi yake ikawa makali. Tunasoma mara nyingi ambapo alilia kwa Mungu kwa huzuni: "Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia. Bwana usikie sauti yangu!" (Zaburi 130:1-2).

Kwa waumini wengi, kuzama kwa chini kunamaanisha mwisho. Wanasumbuliwa sana na kushindwa kwao, wanaendeleza hisia ya kutostahili, na baada ya muda wanahisi kuwa wamefungwa zaidi ya msaada wowote. Isaya aliandika juu ya waumini hao, "Ee uliyeteswa, uliyerushwa na tufani" (Isaya 54:11).

Baadhi hatimaye wakuwa vicha wakimuomba Mungu kwa sababu hawafikiri kwamba anatembea haraka. "Bwana, ulikuwa wapi wakati nilikuhitaji? Nilikulilia wewe lakini haukujibu. Nimejaribu kusubiri lakini sikuona mabadiliko yoyote. "Waumini wengi vivo hivo huachia tu bada ya kujaribu na kujitolea wenyewe kwa dhambi zao. Wengine huingia katika ukungu wa kutojali kwa kiroho, wanaamini kwamba Mungu hawajali tena juu yao: "YEHOVA ameniacha, na Bwana ameniisahau" (Isaya 49:14).

Daudi alitolewa kutoka kwa kina, kwa kukumbuka asili ya msamaha wa Mungu. Baada ya kulilia Bwana, Daudi akaishia kushuhudia, "Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe" (Zaburi 130:4). Roho Mtakatifu alianza kuzunguka roho yake kwa kukumbuka huruma za Mungu na msamaha kutoka kwa Baba, asili ya msamaha.

Kutembea kwa hofu ya Bwana kunatuwezesha kusema, "Najua Baba yangu anipenda na hawezi kamwe kuniacha mimi. Yeye yuko tayari kunisamehe wakati wowote nitakapomwita."

Download PDF