FAIDA ZA TOBA | World Challenge

FAIDA ZA TOBA

David Wilkerson (1931-2011)
April 11, 2018

Tunamjua Danieli kama kijana mwenye nguvu, aliyepewa vipawa ambaye alimtumikia Nebukadneza, mfalme wa Babubuloni kwa uaminifu, na kutafsiri ndoto zake. Lakini matumizi yake makubwa yalikuwa kama matokeo ya kuwa mtu mwema wa sala.

Danieli aliishi maisha ya kujitolea, ya utakatifu ambayo hutaraji kumpata kutubu mbele ya Bwana. Lakini moyo wake ulikuwa anaguswa sana na dhambi na aligundua kwa pamoja dhambi za kutisha za watu wa Israeli. Angalia matumizi yake kwa neno la wingi sisi katika sala yake.

"Tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yak na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi" (Danieli 9:5-6).

"Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, kwa ajili yam lima mtakatifu wa Mungu wangu" (Danieli 9:20). Danieli alikuwa akisema, kwa kweli, "Bwana, shugurika nami wakati unapokuwa unashughulikia watu wako. Ikiwa kuna uovu wowote moyoni mwangu, wutowe nje na uwunionyeshe mimi!"

Je!, kuna faida kwa kutubu? Ndiyo! Faida moja ya ajabu sana ni zawadi ya maono wazi mapya ya Yesu Kristo. Baada ya Danieli kutubu, alipata maono: "Niliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu safi ya ufazi" (Danieli 10:5). Daniel ndiye peke yake aliyemwona huyo mtu, ambaye alikuwa kweli Yesu katika utukufu wake wote!

Kuelewa, Danieli hakuomba kwa ajili ya maono haya; alikuwa tu kutubu, akikiri na kuomboleza juu ya dhambi. Yesu alijitahidi kuja kwa Danieli katika ufunuo huu - Bwana aliianzisha! Unaona, tunapojinyenyekeza mbele za Bwana na kufanya mambo sawa na yeye na wengine, hatuhitaji kutafuta ufunuo. Yesu atajidhihirisha kwetu! Inaweza kuwa si katika maono lakini tutajua kwamba yupo.

Download PDF