HATARI KATIKA ULIMWENGU | World Challenge

HATARI KATIKA ULIMWENGU

David Wilkerson (1931-2011)May 9, 2019

Sauti nyingi kanisa leo zinasema Wakristo wanapaswa kuonyesha aina mpya ya upendo. Wanasema juu ya upendo ambao ukweli wa kibiblia unapaswa kuendana na nyakati. Kulingana na injili yao, hakuna mabadiliko muhimu ya kibinafsi wakati mtu anapokubali Kristo. Hakika, hakuna toba inahitajika. Badala yake, lengo la kuwasilisha injili hii ni kuvunja tu kizuizi chochote kinachoweza kuonekana kuwa kikwazo ili mtu wa Kristo akubaliwe.

Je! Inawezekana kwamba sisi kama Wakristo tumeruhusu uzima wa nuru ya Kristo kuwa sehemu ya giza? Yesu alionya juu ya hatari ya kuruhusu nuru yetu kuwa giza. "Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Tembea wakati mkiwa na nuru hiyo, giza lisije likawapata; maana aendaye gizani hajui aendako" (Yohana 12:35). Kwa mujibu wa Yesu, tamaa lolote linalokubalika kiulimwengu husababisha nuru yetu kuwa giza.

Unaweza kupata urahisi kukubalika ulimwenguni. Watu watakuita rafiki, kukusifu, hata kupenda aina ya injili unayohubiri. Vipi? Inatokea wakati unaruhusu njia za ulimwengu kuingia ndani ya nafsi yako. Unaweza kutupa aibu ya Kristo, unajihakikishia wewe unaweza kuchanganya na giza na bado kuwa mwanga kwa ulimwengu. Lakini haifanyi kazi!

Katika jioni ya mwisho, Kristo aliwaambia wanafunzi wake, "Amri mpya nawapa" (Yohana 13:34). Amri hii mpya haikuhusu njia za uinjilisti. Alikuwa tayari amewambia kwamba wataenda ulimwenguni pote kuhubiri Injili na kuwahakikishia kwamba watahitaji msaada wa Roho Mtakatifu kutimiza amri hiyo. Kwa hiyo amri hii mpya ilikuwa nini? Yesu akawaambia, "Kama nilivyowapenda ninyi ... mpendane vivyo hivyo" (13:34).

"Kwa hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo nin kwa ninyi" (13:35). Upendo wetu kwa kila mmoja katika kanisa lazima tuuonyeshe katika matendo yetu; upendo tu wenye matendo ndiyo utatowa tahadhari kwa kizazi kilichopotea. Ninakuhimiza kumwomba Bwana kwa ubatizo wa upendo ili uweze kuwatumikia ndugu zako na dada zako Wakristo na pia kuleta wengine kwake.

Download PDF