HUPATIKANA KWA NEEMA YA MUNGU | World Challenge

HUPATIKANA KWA NEEMA YA MUNGU

Gary WilkersonDecember 23, 2019

"Mwezi wa sita Malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda katika mji wa Galilaya uitwao Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliochumbiwa na mtu ambaye jina lake ni Yosefu, wa nyumba ya Daudi. Na jina la bikira huyo alikuwa Mariamu. Akaingia nyumbani kwake, akamwambia, Salamu, ewe mpendwa, Bwana yu pamoja nawe! (Luka 1:26-28).

Kisha malaika akatangaza ajabu: "Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kutoka kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba katika tumbo lako na kuzaa mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi” (1:30-32).

Mariamu alikuwa msichana mnyenyekevu kutoka kijiji chenye giza. Kwa kuishi katika tamaduni inayotawaliwa na kiume, alikuwa na matarajio machache katika maisha zaidi ya kuwa mke na mama mzuri. Kwa hivyo fikiria jinsi matarajiyo haa alivyokuwa ya kumushangaza. Malaika akamwambia kwamba amepata neema kutoka kwa Mungu, lakini kidogo sana maishani mwake alionyesha neema ya aina yoyote. Hiyo, hata hivyo, yote ilikuwa karibu kubadilika!

Wengi wetu ni kama Mariamu. Tunapenda kuona hali zetu zikibadilishwa - mtoto anayesumbuliwa akipata kusudi katika Kristo, ndoa yenye wasiwasi imerejeshwa kwa furaha yake ya zamani. Tunapenda pia kuona ukweli tofauti wa kiroho katika ulimwengu unaotuzunguka. Wakati Mariamu alianza kuelewa ukubwa wa ahadi ya Mungu kwake, aliimba wimbo wa kutowa shukrani na sifa: "Nafsi yangu inamtukuza Bwana, na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, kwa kuwa ameutazama unyonge wa mtumwa wake mnyenyekevu. Kwa maana tazama, tangu sasa vizazi vyote vitaniita mbarikiwa” (1:46:48).

Ziara kutoka kwa malaika haikuwa tukio la kihemko, la wakati mmoja kwa Mariamu. Hapana, ilikuwa ukweli wa kumfunga na maisha yake yalibadilishwa milele. Vivyo hivyo, unapopata kibali cha Mungu, haileti mabadiliko ya kihemko tu. Mungu huzaa kitu kipya katika maisha yako, anabadilisha kabisa kozi yako, na husababisha wimbo mpya ndani ya roho yako.

Leo, unaweza kudhani Mungu hayupo, lakini neema yake iko kwako! Anachukua kitu kipya, kubadilisha jaribio lako kuwa utukufu wake. Ana mkono wake juu yako, kwa hivyo mwamini kwa moyo wako, familia yako, hali yako - na utaona utukufu wake.

Download PDF