JE! UNAJUA KAMA KRISTO ANAISHI NDANI YA MOYO WAKO? | World Challenge

JE! UNAJUA KAMA KRISTO ANAISHI NDANI YA MOYO WAKO?

Gary Wilkerson
July 9, 2018

"Hamujui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la mungu, na kuwa roho wa Mungu anakaa ndani yenu?" (1 Wakorintho 3:16-17).

Paulo anaanza sehemu hii ya barua hii kwa kuuliza, "Je, hamujui?" Ni swali kidogo la kutisha kwa sababu Wakristo wa Korintho walikuwa karibu miaka minane katika imani yao, lakini anawauliza mojawapo ya msingi wa maswali . "Hamujui kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu?" Labda hawakuweza kuzingatia ukweli huo ingawa Paulo alikuwa amefundisha hapo awali.

Ninataka kuuliza swali hili. Unajua kweli kwamba wewe ni hekalu la Mungu? Je! Una uhakika? Je! Imewekwa ndani ya moyo wako? Mungu huyu anaye ishi ndani yetu katika mwanga usiosogelewa, wa utukufu, wa ajabu, wa thamani, wa upendo, safi, na mtakatifu aliyechaguliwa mahali pa kuishi na ni katika wale ambao nyoyo zao hunyenyekea na anaye uzunishwa.

Je, Inaathirije kujua kwamba Mungu huyu wa viumbe vyote anaishi ndani yako? Je, hilo linafanya nini kwa matatizo yote na migogoro ambayo unakabiliwa nayo katika maisha? Majaribio na dhiki unayopitia? Uchungu wa maisha yako? Maumivu?

Kristo anaishi ndani yenu, uwepo wa dhahiri wa Mungu. Moto wa Mungu uliowaongoza na kuwaelekeza wana wa Israeli, ameamua sio kwenda nje tu mbele yako, lakini akasema, "Subiri dakika! Nikumbatie au nitakuja kwako na kuishi ndani yako." Nguzo ya moto, wingu, moshi - anaishi ndani yako sasa. Mwelekeo, uongozi, uwezo, nguvu, utukufu, upendo, matunda ya Roho.

Tunahitaji kuomba Roho Mtakatifu kutusaidia kutaja Mungu katika maisha yetu, katika uzoefu wetu wa ibada, katika safari yetu ya kila siku pamoja naye.

Download PDF