JE! UNAZUBAA KATIKA IBADA? | World Challenge

JE! UNAZUBAA KATIKA IBADA?

David Wilkerson (1931-2011)December 19, 2019

Ninataka kuzungumza nawe juu ya usumbufu wa akili wakati wa sala na kuachwa kwa ibada - haswa katika nyumba ya Mungu. Yesu aliwaita watu wanafiki ambao walikuja mbele Yake kwa maneno ya sifa, lakini akili zao na mioyo yao zilikuwa kwenye shuguli nyengine. Alizungumza nao moja kwa moja, akisema, "Unanipa kinywa chako na midomo yako - lakini akili yako iko mahali pengine. Moyo wako hauko karibu na Mimi!"

Na wewe je? Uwezekano mkubwa zaidi, unakuwepo katika nyumba ya Mungu kwa saa moja kila wiki. Kwa hivyo, mwili wako uko kanisani - lakini akili yako iko wapi? Mdomo wako unasema, "Nakuabudu, Bwana" - lakini moyo wako uko mbali sana kutoka mita elfu? Je! Mawazo yako yanakuelekeza wapi wakati wa ibada na sifa?

Sio jambo rahisi kuingia ndani ya nyumba ya Mungu kumwabudu! “Musa akamwambia Haruni; Hivi ndivyo BWANA alivyosema, akisema, Nitatakaswa mimi katika hao wanikaribiao, nami nitatukuzwa mbele ya watu hao wote'' (Mambo ya Walawi 10:3). Mungu alikuwa amemwambia Musa, "Sitatendewa kama mtu wa kawaida! Ikiwa utaka kuja mbele yangu, lazima uje mbele yangu ulisha jitakasa. Wote wanaokaribia utakatifu wangu lazima wafanye hivyo kwa uangalifu na uzingatiaji - kwa sababu ya utukufu wangu na ukuu."

Hatupaswi kusema chochote katika uwepo wa Bwana bila mioyo yetu na roho ndani yake. Yesu anaamuru, "Mungu ni Roho, na wale wanaomwabudu lazima wamwabudu kwa roho na ukweli" (Yohana 4:24).

Nyumba ya Mungu ni nyumba ya ibada. Tunapoingia, tunapaswa kuweka kando miili yote na kulia, "Bwana, siko mahali nilipaswa kuwa lakini ninakupenda! Weka ukuta wa moto kuzunguka mawazo yangu na wacha nikuleteye sadaka ya sifa na yenye kusudi kamilikwa kukutukuza!"

Mungu anakupenda na anajua nguvu ambayo ibada safi huondoa ndani ya roho yako. Inakufanya uwe na nguvu kuliko simba na kubwa kuliko jitu kubwa, ukivutia chini kila ukuta na ngome inayokuja dhidi yako. Haleluya!

Download PDF