JE! WEWE UKO SHAHIDI KATIKA JIJI LAKO? | World Challenge

JE! WEWE UKO SHAHIDI KATIKA JIJI LAKO?

David Wilkerson (1931-2011)October 25, 2019

Mara nyingi tunatarajia Mungu kutembea katika moja wapo ya njia mbili: ama kwa kumiminwa kimaajabu kwa Roho wake Mtakatifu ili kufagia umati katika ufalme wake, au kwa kutuma hukumu kuwaleta watu kwa magoti yao au hata kuwaangamiza. Lakini, wapenzi, hiyo sio njia ya Mungu ya kubadilisha mambo katika siku hizi mbaya. Njia yake ya kujenga magofu kila mara imekuwa ni kutumia wanaume na wanawake wa kawaida ambao amewagusa. Na yeye hufanya hivyo kwa kuwajaza Roho wake Mtakatifu na kuwatuma kwenye vita wakiwa na imani kubwa na nguvu! "Wote walijazwa na Roho Mtakatifu" (Matendo 2:4).

Wewe uko shahidi wa Mungu kwa mji wako! Yeye hutumia watu ambao hukaa peke yake naye, kumtafuta katika maombi, kutoa mioyo yao na kisha kwenda kamili ya Roho Mtakatifu, imani na nguvu. Ikiwa Mungu hajakutumia, inawezakana ni kwa sababu hauwezi kutumiwa. Hiyo inatokea wakati waumini “wanashikwa wakitazama utukufu” badala ya kuandaa kutumiwa.

Wanafunzi walikaa kwenye utukufu wakati Yesu alipochukuliwa mbinguni. Wangeweza kusimama hapo milele, wakifurahia mwangaza wa joto, lakini malaika wa Bwana akawakemea kwa upendo: "Je! Kwa nini mmesimama mukitizama mbinguni? (Matendo 1:11). Kulikuwa na maandalizi mengi aliohitajika na majukumu ya kukamilika. "Walirudi Yerusalemu ... wakaenda katika chumba cha juu… [na] hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kuomba" (Matendo 1:12-14).

Unapoibuka kutoka kwa kumtafuta Mungu, unaweza kusimama kwa ujasiri mbele ya wafanyikazi wenzako, familia, mtu yeyote, na ushahidi wako utaonyesha moja ya athari mbili: toba ya kweli au hasira yako. Kwa njia yoyote, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, utaongea neno "ambalo huingia mioyoni."

Nenda mbele Zaidi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ukibeba nuru ya Yesu kila mahali uendako.

Download PDF