JE, YESU BADO ANAFANYA MIUJIZA? | World Challenge

JE, YESU BADO ANAFANYA MIUJIZA?

Gary WilkersonJuly 8, 2019

Neno la Mungu linajaa hesabu ya umati wa watu ambao wanakuja kwa Yesu ili waponywe. "Na habari zake zikaenea katika Siria yote; wakamletea wagonjwa wote, wale waliokuwa na magonjwa na maumivu mbalimbali, wenye pepo mbaya, na wenye kifafa, na wenye kupooza; na akawaponya" (Mathayo 4:24).

"Wakamletea wengi ... naye akawatoa pepo kwa neno na akaponya wote waliokuwa wagonjwa" (8:16).

"Alipofika pwani akaona umati mkubwa, naye akawahurumia na kuwaponya wagonjwa yao" (14:14).

Kwa nini miujiza hii ilifanyika? Kwa sababu Yesu aliwaona watu ambao walikuwa wagonjwa na walioteseka na alikuwa na hurumia juu yao. Alipokuwa akiwaangalia wale waliopotea, moyo wake ulikuwa umevunjika mara kwa mara kwa waathirika. Mbali na huruma yake kubwa, Yesu alikuwa na wito mkubwa juu ya maisha yake - utukufu wa Baba yake. Alitaka kuonyesha ukubwa na utukufu wa Mungu na kuinua jina lake kwa njia ya kazi alizofanya.

Wanafunzi walipokuwa wakitembea pamoja na Yesu, na kufanya huduma bega kwa bega wakiwa naye, Yesu alisisitiza kwao kwamba wanaweza kufanya mambo makuu zaidi kuliko yeye. "Kwa kweli, nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya" (Yohana 14:12).

Sasa, wewe na mimi tunaamini kwamba Yesu huponya wagonjwa na alikuja kufikia waliopotea. Lakini, Je! Tunamwona akifanya miujiza kupitia kwetu? Tunaimba nyimbo za Yesu, tunasikia mahubiri ya Yesu, kusoma vitabu vya Yesu na kuombeyana - lakini tunamfuata Yesu kwa karibu? Kwa kiasi kikubwa ca mawazo ya wamarekani wengi wanasema kwamba kufuata Yesu kunamaanisha kuamini imani fulani - lakini kumfuata kwa bidii ni wingi wa zaidi.

Ombeni sala hii pamoja nami: "Yesu, nipe nguvu, imani, ujasiri, ujasiri wa kuchunguza moyo wangu kwa Neno lako. Kisha nifarijie kukuruhusu kufanya kazi kupitia mimi hata kazi kubwa zaidi kuliko ulizofanya wakati ulipokuwa duniani."

Download PDF