JUHUDI ZA KRISTO | World Challenge

JUHUDI ZA KRISTO

Nicky CruzJune 1, 2019

"Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida" (Wafilipi 1:21). O, kila mmoja wetu anaweza kuwa na shauku ya kuishi kwa ajili ya Kristo iliyojaza Paulo. Moja kwa moja - kwa uongozi wa Roho Mtakatifu - alieneza Ukristo katika Dola ya Kirumi. Hakuwa na wasiwasi ikiwa angeishi au kufa, alitaka kuendeleza ufalme wa Mungu.

Wakristo leo wameendeleza imani ya uongo - imani bila kujitolea. Tunashugulikia kwa kimbilia  kufanya mikutano ya Bibilia na mafundisho, tunatafuta wasemaji wengi wa busara wa Biblia, na tunaendesha masomo ya Biblia kila wiki ili kujaza vichwa vyetu maelezo mhimu zaidi na fomu. Wakati huo huo, mamilioni ya watu wanaoumizwa duniani kote wanakufa bila matumaini. Tumeitwa kuwafikia.

Je! kujitoa kumanisha nini kwa yote? Ina maanisha tu kujisalimisha kwa Bwana na kazi yake. Tunashikiliwa na kazi mbele yetu, licha ya hali nyingi. Ina maanisha kufundisha darasa la Jumapili kila Jumapili - bila kujali nini - na kuruhusu watoto katika darasa hilo wawe vijana muhimu zaidi ulimwenguni. Inamaanisha kuwaombea kwao na kuchukua muda wakati wa wiki ili kujua nini kinachowasumbuwa.

Kujitolea hakuzingatie urahisi, au mabadiliko ya hisia za hisia. Dhamira ya kweli bado ni jambo la kudumu, ambayo inaweza kuhesabiwa. Kwa kusikitisha, Wakristo wengi hawajui jinsi ya kujitolea kikamilifu kwa Bwana. Wao pia hupatikana katika maisha yao wenyewe. Na wengi wanapenda kuwa na furaha katika kanisa - sio kujitolea.

Tunakimbilia kwenye hatari ya kuwa kama kanisa la Laodikia liliyotajwa katika kitabu cha Ufunuo – sio baridi wala moto, Wakristo wasio na kitu. "Nayajua matendo yako, kwamba wewe hu baridi au hu moto. Ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu wewe hu baridi au hu moto ... Nitakutapika kutoka kinywa changu" (Ufunuo 3:15-16). Omba Bwana afanye upya roho ya kujitolea ndani yako ili uwe mtumishi aliyejitolea ambaye yeye anataka uwe.

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana, na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka (Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco: Kimbiya, Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).

Download PDF