KITU KILICHOONGEZWA KATIKA MOYO ULIOGEUKA | World Challenge

KITU KILICHOONGEZWA KATIKA MOYO ULIOGEUKA

Gary WilkersonSeptember 2, 2019

"Mwana- sharia mmoja ilisimama ili amjaribu, akisema, Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?" (Luka 10:25). Waandishi na Mafarisayo walikuwa wamekutana na Yesu, na kutowa changamoto kwa mamlaka yake mara nyingi lakini sasa mwana- sheria alimwendea, labda mtu aliyetumwa nao. Wana-sheria wamefunzwa vizuri katika sanaa ya mijadala na bila shaka huyu pia alikuwa na sifa nzuri katika sheria za Agano la Kale. Labda alitarajia Yesu aanze kurudia baadhi ya sheria kuhusu Sabato, kuosha mikono, chakula safi na chafu. Sheria nyingi! Na ni ipi inayoongoza kwenye uzima wa milele?

Yesu alijibu swali la mwana-sheria na swali: "Ni nini kilichoandikwa katika torati? Unasoma nini?” (10:26). Mwana-shera akajibu, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe" (10:27). Yesu akamjibu, "Umejibu kweli; fanya hivi nawe utaish” (10:28).

Na maneno hayo rahisi, Yesu aliondoa mzigo wa sheria na kanuni zote na akawasilisha ujumbe wenye kuburudisha zaidi ulimwengu unaobadilika, ujumbe ambao unaweza kubadilisha hujawahi kusikia.

Yesu alitaja jambo la muhimu zaidi kwanza: umpende Mungu kwa moyo wako wote, roho na akili. Na baada ya kuingia katika uhusiano na yeye, atakupa moyo mpya, moyo ambao unaweza kuhamasishwa na huruma kwa wengine. "Nami nitatoa moyo wa jiwe iliomo ndani ya mwili wenu, na kuwapa moyo wa nyama" (Ezekieli 36:26). Moyo wa fadhili na kujali wengine.

Kamwe huwezi kumpenda jirani yako kama vile Yesu anatupenda, lakini kupenda wengine ni uvumbuzi wa asili wa moyo uliobadilika. Anapokugeuza, unaweza kusema kama mtunga-zaburi, "Kufanya mapenzi yako, Ee Mungu, ndiyo furaha yangu; Naam, sharia yako imo moyoni mwangu” (Zaburi 40:8).

Download PDF