KUBURI KILICHOJERUHIWA | World Challenge

KUBURI KILICHOJERUHIWA

David Wilkerson (1931-2011)June 6, 2019

Kwa majadiliano yote katika kanisa kuhusu msamaha, kurejeshwa, na uponyaji, kidogo sana inaonekana kuwa imeonyeshwa kweli na Wakristo. Sisi sote tunapenda kufikiria wenyewe kama watu wa amani, wainuwaji wa walioanguka, daima kusamehe na kusahau. Lakini hata wale wenye wanaingiya kiroho wana hatia ya kutoonyesha roho ya msamaha.

Tunaona kama ni vigumu kuwasamehe wale ambao wamejeruhi kiburi chetu; au mtu asiye toa shukrani; au mtu yeyote anayetudanganya. Na wengi wa Wakristo hawajui jambo la kwanza kuhusu kushughulikia upinzani. Tunatumia mbinu zote za kuficha chuki zetu, kuwa na uwezo wa kuimarisha ulinzi wetu kwa ujasiri. Ndiyo, kiburi kilichojeruhiwa ni jambo lenye kutisha.

Mara nyingi, kabla ya kuwasamehe wengine, tunapaswa kujifunza kumsamehe Mungu. Ingawa Mungu hajawahi kutenda dhambi kwa mtu yeyote, hilo halituzuia kushikilia chuki dhidi yake. Tunakuja mbele yake kwa kuomba, lakini tunaendeleya kushikilia hisia mbaya kwa yeye kwa sababu tunadhani kwamba hakufanya chenye tunafikiria kama lazima angekifanya. Sala inaweza kuwa haijajibiwa kwa wiki, miezi - hata miaka. Au ugonjwa usiyotarajiwa hutokea au msiba kubeba mtu mpendwa - na hapo hapo imani huanza kuyumba yumba.

Kumbuka, Neno la Mungu linaeleza wazi kwamba mtu mwenye kuyumba yumba hawezi kamwe kupokea kitu chochote kutoka kwa Mungu: "Ila aombe kwa imani, pasipo na shaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la baharini linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu huyo asithani kwamba atapokea kitu chochote kutoka kwa Bwana. Mtu mwenye nia mbili husita-sita katika njia zake zote" (Yakobo 1:6-8).

Yesu alielewa tabia hii yenye kuwa ndani ya watoto wake ya kushikilia chuki dhidi ya mbinguni wakati milima haiondolewe kwenye ratiba. Alimuonya Petro asiulize kitu chochote akiwa amesimama mbele ya Mungu mpaka isipokukuwa amesamehe. "Kila msimamapo na kuomba, mkiwa na neno dhidi ya mtu yeyote, mumsamehe; ili Baba yako aliye mbinguni awasamehe makosa yenu" (Marko 11:25).

Ikiwa una chuki yenye siri katika moyo wako dhidi ya mtu mwingine au dhidi ya mbinguni, basi acha Roho wa msamaha amiminike kupitia kwako. Mungu ni mwaminifu!

Download PDF