KUELEKEZA MACHO KWA YESU | World Challenge

KUELEKEZA MACHO KWA YESU

David Wilkerson (1931-2011)August 16, 2019

"Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiaaga mkutano. Naye alipokwishwa kuwaaga mkutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.” (Mathayo 14:22-24).

Kufuatia muujiza wa kuwalisha wale elfu tano, Yesu aliwacha watu waende zao na kuwaambia wanafunzi wake waende pia. Ilikuwa siku ngumu na Mwalimu alitaka kupumzika kidogo. Lakini mashua ya wanafunzi ilishikwa na dhoruba, na ingawa walikuwa mabaharia wenye uzoefu, ukali wa dhoruba hiyo ulisababisha kelele. Walizani kama wangepata faraja kwa sababu Yesu alikuwa karibu, lakini hawakutarajia kitakachofuata.

"Yesu akawaendea kwao, akitembea juu ya bahari. Na wanafunzi walipomwona akitembea juu ya bahari, walifadhaika, wakisema, "Ni pepo!" (Mathayo 14:25-26). Kwa kweli, wanafunzi waliogopa, lakini Petro alichukua hatua ya ujasiri wa imani na kuacha mashua. Mawono kwa Mwokozi wake yalitosha kwake! "[Petro] akasema, 'Bwana, ikiwa ni Wewe, niamuru nije kwako juu ya maji'” (14:28). Kwa hivyo, akielekeza macho yake wazi kwa Yesu, Petro alichukua hatua hiyo kutoka kwenye mashua. Hakuwa anaonyesha imani yake au kujaribu kudharau mtu yeyote, alitaka tu kuwa karibu na Bwana wake.

Wakati ni kweli kwamba Petro alizama wakati alipoondoa macho yake kwa Bwana, aligundua mahali pa Kristo juu ya bahari ya dhoruba na ya mawimbi. Alikuwa akitembea juu ya kile kilichomtishia kufika kwa Yesu. Imani ambayo ilimfanya awe juu ya yote kwa muda ingeweza kumuweka milele. Lakini aliondoa macho yake kwa Kristo na aliruhusu machafuko yaliyokuwa yakimzunguka kutuliza ujasiri wake.

Hadithi ya Petro inatukumbusha kwamba hali mbaya zaidi, Mkristo anahitaji sana kufuata Kristo. Naomba uangalie usoni mwake katikati ya shida yako na uombe, "Nitenge karibu nawe, Bwana. Acha kila kitu maishani mwangu kinielekeze kwako!”

Download PDF