KUINUKA KATIKA UMOJA | World Challenge

KUINUKA KATIKA UMOJA

Nicky Cruz
February 3, 2018

Nini ikiwa Mwili wa Kristo kwa ujumla unaweza kuja pamoja kwa umoja, kuacha tofauti zetu za maoni na migogoro yetu ya kijamii na mafundisho, na kutazama lengo moja tu – la kufikia waliopotea? Nini kama tuliomba Roho Mtakatifu kuponya majeraha na kuleta msamaha kwa mioyo na roho zetu, kusahau ya zamani na kuzingatia ya baadaye? Ni ufufuo gani wa kiroho ambao ulimwengu unaona wakati wanatuwona sisi, tukisimama pamoja mbele yao tukiwa na umoja?

Hiyo ndio aina ya upendo na umoja ambao Yesu aliomba kwa kabla ya kwenda msalabani: "Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, name ndani yako, hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe iliyenituma. . . . Ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ilivyonipenda mimi" (Yohana 17:20-23).

Yesu aliomba kwa umoja kati ya wafuasi wake kwa sababu alijua kwamba bila ya hayo tutakuwa bila msaada katikati ya dunia yenye hasira na chuki. Ni kwa njia ya roho ya umoja, kwa kuimarisha pamoja kama moja dhidi ya mashambulizi ya Mwovu, kwamba tuna uwezo wa kuleta ujumbe wa Mungu wa upendo na matumaini kwa ulimwengu uliojaa dhambi. Hatuwezi kutoa amani na upendo kwa utamaduni wa machafuko kama hatuwezi kuwa ndani ya viwango vyetu.

Ninatamani kuona siku ambapo Wakristo kila mahali "huinuka katika umoja" na kuuliza kila mtu katika sayari hii, ili pawe kuinama magoti mbele ya Mwokozi wetu mwenye huruma. Hiyo itakuwa siku ya watu bila kamwe kusahau - siku ambayo wafuasi wa Yesu watakuja pamoja na moyo mmoja, mawazo moja, Roho mmoja, na kusudi moja: na kutowa moto mtakatifu mmoja duniani.

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwa maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza ya kuokoka kwake ulisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinacho chomoka (Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuliuzwa vizuri, kiitwaco:Kimbiya, Mtuto, Kimbiya (Run, Baby, Run).

Download PDF