KUJISALIMISHA: KUJITOA KWA YESU | World Challenge

KUJISALIMISHA: KUJITOA KWA YESU

David Wilkerson (1931-2011)October 12, 2018

Kujisalimisha. Kwa maneno halisi, kujisalimisha kuna maana ya kutoa kitu kwa mtu mwingine. Pia inamaanisha kuacha kitu kilichotolewa kwako - mali yako, nguvu, malengo, hata maisha yako.

Wakristo husikia mengi kuhusu maisha ya kujisalimisha, lakini inamaanisha nini? Uhai wa kujisalimisha ni tendo la kumrudia Yesu maisha aliyowapa. Ni kuacha kabisa maisha yako juu ya mikono yake ya kufanya nawe kama atakavyotaka.

Yesu mwenyewe aliishi maisha ya kujisalimisha: "Kwa maana nimeshuka kutoka mbinguni, si kufanya mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi ya yule aliyenituma" (Yohana 6:38). Kristo hakufanya chochote mwenyewe; hakuwa na hoja na hakuzungumza neno bila kufundishwa na Baba. "Mimi si fanyi neno kwa nafisi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.  Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; Kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo" (Yohana 8:28-29).

Kujisalimisha kwa Yesu kwa Baba ni mfano wa jinsi sisi wote tunapaswa kuishi. Unaweza kusema, "Yesu alikuwa Mungu katika mwili; maisha yake yalitolewa kabla hata kuja duniani. "Lakini maisha ya kujisalimisha sio yakulazimishwa kwa mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na Yesu.

Hakuna mtu analazimishwa kutoa maisha yake kwa Mungu. Ukweli ni kwamba, tunaweza kuwa na mengi ya Kristo kama tunavyotaka. Mtume Paulo alijua jambo hili na alichagua kufuata mfano wa Yesu wa maisha ya kujitolea kikamilifu. Zamani alikuwa anajifanya mkamilifu kwa kuchukia Yesu na kutesa wa Wakristo, alisema kuwa aliwachukia wafuasi wa Kristo. Alikuwa mwenye elimu sana, mtu mwenye mapenzi ya kibinafsi na tamaa, aliongoza kwa mafanikio. Hata hivyo Bwana alichukua mtu huyu aliyejitengeneza mwenyewe, aliyejitambulisha, anayeongozwa na kumfanya awe mfano mkali wa maisha ya kujisalimisha. Paulo akawa mmojawapo wa watu anaotegemea Mungu, mtu aliojazwa na Mungu, alioongozwa na Mungu katika historia yote.

Paulo alitangaza maisha yake kuwa mfano kwa wote wanaotaka kuishi kikamilifu kwa Kristo: "Lakini kwa kwa ajili hii nilipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristoaudhihirishe uvumulivu wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele" (1 Timotheo 1:16).

Download PDF