KUKAMILISHWA NA UPENDO | World Challenge

KUKAMILISHWA NA UPENDO

David Wilkerson (1931-2011)November 12, 2019

Upendo, hofu, utii – wakati vinapokuja kwa ajili ya kutembea na Mungu, havitenganishwi kwa sababu huwezi kufanya mazoezi moja bila yangine ma wili.

  • Hofu - "Kumcha Bwana ni kuchukia uovu" (Mithali 8:13).
  • UPENDO - "Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye" (Yohana 14:21).
  • Utii - "Na huu ndio upendo: kwamba tuenende kwa kuzifuata amri zake" (2 Yohana 6).

Huwezi kumpenda Mungu bila kuwa na hofu ya Mungu ndani yako; huwezi kumpenda bila kutii Neno lake. Wengine hufundisha kuogopa Mungu tu ndio kunawawezesha waumini kukimbia dhambi, wakati wengine hufundisha kwamba msukumo mzuri tu dhidi ya dhambi ni upendo. Kumpenda kunamaanisha kutii kila amri yake, lakini ni nini huleta utii thabiti na wa kudumu? Utii wa kimungu, upendo unatokana na chanzo kimoja: hofu ya Mungu aliye hai. Utii unaowekwa na hofu ya kweli na ya ucha Mungu ni upendo umekamilika.

Ikiwa kweli unayo hofu ya Mungu ndani yako, basi utatii kila neno lake. Unapata hofu ya Mungu kama Israeli alivyofanya: unajifunza! Bwana yuko tayari kufundisha woga wake kwa wote wanaoutaka: “Njooni, enyi watoto, mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha Bwana” (Zaburi 34:11). Baba yetu mwenye upendo anatufundisha kumwogopa kupitia Neno lake.

Yesu aliahidi baraka za ajabu kwa wote wanaomtii. "Naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake" (Yohana 14:21). Hii ni moja ya ahadi zenye nguvu katika Neno la Mungu! Baba ana upendo maalum moyoni mwake kwa wale wanaotembea kwa utii kwa ajili ya Mwana wake.

Anza kutembea kikamilifu katika utii kwa yote amabayo unaofahamu maagizo yake na utakamilika katika upendo wako kwa ajili ya Yesu!

Download PDF