KULINDA MAISHA YAKO YA MAOMBI | World Challenge

KULINDA MAISHA YAKO YA MAOMBI

David Wilkerson (1931-2011)February 14, 2020

Tumesikia mazungumzo ya njama miaka yote lakini kuna njama moja tu ambayo inayohusu Baba yetu wa mbinguni - mpango uliolenga moja kwa moja kwa Wakristo ambao wameweka mioyo yao kuingia utimilifu wa Kristo. Njama hii ina maana ya kuzuia mpango wa Mungu wa kuongeza jeshi la watu waliotakaswa - wanaume na wanawake waliojitolea kabisa kwa ukuu wa Yesu katika maisha yao. Acha tuiite njama ya usumbufu.

Ibilisi huwaogopa Wakristo ambao wana njaa na kiu ya haki. Kwa kweli, anaogopa waombaji watakatifu kuliko vile anaogopa miaka elfu kwa minyororo. Kuomba kwenye nguvu kwa mwombezi mmoja husikika kama mngurumo mkali katika milango ya kuzimu. Ndio maana Ibilisi hufanya kazi kwa bidii ili kuvuruga na kuingilia mfuasi wa Kristo kama huyo.

Mojawapo ya najama ya adui ni kuonesha mahitaji ya kibinadamu ambayo anataka umakini wetu. Tunalia, "Bwana, nawezaje kugeuza na kuwacha wale ambao wanaumia?" Jibu kutoka kwa Bwana ni, "Unawezaje kunipuuza?" Hii ndio habari ya hoja.

Je! Kuna mtu yeyote au kitu chochote kinachoweza kuwa muhimu sana kwetu kuliko Bwana wetu? Je! Haja yoyote au kuumiza hutuzuia kukutana na Bwana mwenyewe? Hata Yesu aliachana na hitaji kubwa la wanadamu karibu naye ili aweze kuzungumza kimya kimya na Baba yake wa mbinguni. Inakuja wakati katika maisha ya kila Mkristo anapaswa kusema, "Unaweza kusubiri. Nimerudi lakini kwanza lazima nitumie wakati katika maombi. Nafsi yangu ina njaa na lazima nikulishe Neno la Mungu. Ikiwa sipati wakati peke yangu na Bwana, sina chochote cha kukupa ila huruma dhaifu ya wanadamu."

Ili kulinda wakati wako wa maombi na kuhimili njama zote za Shetani, unaweza kufanya mambo matatu:

  1. Fanya ushirika na Bwana kuwa lengo lako la msingi maishani. Ayubu alisema, "Nimeyatunza maneno ya kinywa Chake kuliko chakula changu" (Yobu 23:12).

  2.  Fikiria miadi yako pamoja na Mungu takatifu zaidi kuliko miadi yoyote na watu - haijalishi wao ni nani!

  3.  Kataa kila usumbufu ambao uko ndani ya uwezo wako na uchukue mamlaka ya kiroho juu ya usumbufu huo unaotambua kuwa wa kawaida.

Ingia katika utimilifu wa matembezi yako na Kristo, kama Mungu alivyopanga kwako.

Download PDF