KUPONYA NAFSI HII YENYE SHIDA | World Challenge

KUPONYA NAFSI HII YENYE SHIDA

David Wilkerson (1931-2011)March 23, 2018

Mchungaji kijana aliniita, alikuwa tayari kuacha huduma. Bwana alikuwa amemtumia kwa njia ya ajabu, lakini sasa alikuwa amevunjika moyo, akijisikia kuwa hana maana, hakuwa na faida kwa Mungu hata kidogo. Aliponiita, alipigwa na butwaa juu ya maamuzi fulani aliyoyafanya na alionyesha kwamba alikuwa tayari kuacha. Alikuwa na hasira kwa Mungu na wakati alipokuwa akizungumza nami, nilihisi kwamba alitarajia kuwa na hasira naye. Lakini alikuwa amevunjika moyo sana na kupigwa chini kwamba nilihisi upendo na huruma peke yake vya Mungu viwe juu yake.

Sikumufundisha mchungaji kijana huyu au kumkemea. Badala yake, niliomba kwa kimya, "Bwana mpendwa, ninaweza kusema nini kwa mtu huyu utakayoponya nafsi yake? Una nini kwa ajili yake? Ni faraja gani kutoka kwa Roho wako, Neno lako?"

Bwana alinisisitizia, "Mtume kwa Zaburi ya 107." Baadaye niligundua kuwa Zaburi hii imekuwa inaitwa "karamu ya upendo wa Agano la Kale." Ni mojawapo ya vifungu vyenye moyo zaidi katika Neno la Mungu na lina maana hasa kwa wale wanaohitaji msamaha, ukombozi, kurejeshwa. Aya ya mwisho imeahidi msomaji kuelewa kwa kweli Mungu ni nani:

"Aliye na hekima na ayaagalie hayo; na wazitafakari fadhili za Bwana" (107:43).

Mungu anasema, "Angalia, soma, soma Zaburi hii na utapewa ufahamu kamili wa uvumilivu wangu na huruma." Naamini kwamba unaposoma Zaburi hii yote, utapata ufunuo wa upendo mkuu wa Mungu, hata unaelekea kwa uwaasi na kusiotii. Unaona, ni ahadi – ni ushahidi kwamba Mungu hawezi kutembea nje ya yeyote kati ya watoto wake, bila kujali ulefu wa kwenda chini walio dumbukia.

Fikiria jinsi unavyopenda mtoto wako mwenyewe. Je, kuna chochote cha thamani ambacho mtu anaweza kufanya ambacho kitakufanya umkatae? Ni marangapi Baba wa mbinguni anapenda zaidi sana mwenyewe na huongeza upendo na msamaha! Sikio lake hufunguliwa kwa kilio chetu daima.

Download PDF