KUPUMZIKA KATIKA UPENDO WA MUNGU | World Challenge

KUPUMZIKA KATIKA UPENDO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)March 19, 2020

Mungu anatuambia, "Mwanangu, nipe moyo wako" (Mithali 23:26). Upendo wake unatutaka tuweze kurudishiwa, kwamba tumrudie kwake upendo uliokamilika, usiotengwa, unaohitaji moyo wetu wote, roho, akili na nguvu zote. Lakini, Bwana anatuambia bila shaka, "Hauwezi kupata upendo wangu. Upendo ninaokupa haujaustahili. "Yohana anaandika, "Tunampenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza" (4:19).

Hakuna mtu anayeamka siku moja na kuamua kuachana na dhambi na kumfuata Yesu. Hapana, Roho Mtakatifu wa Mungu anafikia jangwa la maisha yetu, anatuonyesha hali yetu ya kupotea na kutufanya tuhuzunike katika dhambi yetu. Baba yetu alitutumia Neno lake ili kutuonyesha ukweli, akatuma Roho wake ili atudhibitishie, na baadaye akaja nyuma yetu yeye mwenyewe. Alifanya yote kwa ajili yetu!

Dawudi anaelezea kupumzika katika upendo wake kwa Mungu, wakati alipoaandika, "Ni nani niliye naye mbinguni,Wala duniani ninatamani ila Wewe tu” (Zaburi 73:25). Moyo unaompenda Bwana huacha kabisa kutazama mahali pengine kwa faraja. Badala yake, hupata kuridhika kamili ndani yake. Fadhili za Mungu ni bora kuliko maisha yenyewe.

Moyo kama huo pia unafurahiya upendo wake kwa Mungu. Wakati mtoto wa Mungu anajua ni kiasi gani Baba yake anampenda, inaweka raha katika nafsi yake. Upendo wetu kwa Baba lazima uchukuliwe kupitia Mwana wake. Yesu anasema, "Hakuna mtu anakuja kwa Baba isipokuwa kupitia mimi" (Yohana 14:6). Ni kwa Kristo pekee kwamba tunakubaliwa na Baba na kuingia kupitiya kwake.

Mungu aliweka wema wake wote, upendo, rehema na utukufu kwa mtoto wake na alimtuma Yesu kudhihirisha na kutufunulia utukufu huo. Kwa hivyo, Kristo anakuja kwetu kama taswira ya Baba yetu mwenye upendo. "Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami pia nilivyowapenda ninyi; kaeni katika upendo wangu” (Yohana 15:9).

Unapopata urafiki wa kweli na Baba, utaweza kutembea katika utukufu wake - siku zote za maisha yako!

Download PDF