KUPUUZA ZAWADI NJEMA YA MUNGU | World Challenge

KUPUUZA ZAWADI NJEMA YA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)March 8, 2018

Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu na kutoka mahali patakatifu ndani ya moyo wako, anapumua ushawishi wake juu ya hisia zako zote - kusisimua, kuhimiza, kufariji, kuongoza, kuhukumu, kudhihirisha ukweli wa Kristo. Ni zawadi ya ajabu!

Kwa kusikitisha, wengi hupuuza zawadi hii nzuri sana ndani yetu. Na wengine hupuuza Roho wa Mungu kabisa, wakienda maisha yao ya kila siku ikionekana kwamba haishi ndani yao.

Mpendwa, zawadi ya Roho Mtakatifu ndani yetu hutupa nguvu zote, rasilimali, matumaini, neema na amani tutakayohitaji. Na bado kwa kweli sisi tumewekwa chini yake kwa uoga wa unyanyasaji mbaya wa kupuuzia. Ndiyo, ni unyanyasaji dhidi ya Roho kwa ajili yetu tukibeba mizigo isiyohitajika – na kutembea mbele ya ulimwengu mwovu unaoteketea na kutenda kama Mungu wetu amekufa.

Tunapaswa kuwa ushuhuda kwa wale walio karibu nasi na kama huna kukimbilia kwa Bwana kwa maswali yako na mizigo, basi ulimwengu una haki ya kukuuliza, "wapi Mungu wako? Wapi Kristo unayezungumzia sana kuhusu?"

Tunapaswa kuwa ushahidi wa kutosha wa kuwepo kwa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Huu umepotea ya kizazi kilichopotea, kilichovunjika, kilichochanganyikiwa kinahitaji kuona na kutusikia sisi kutangaza, "Roho yangu iko katika mapumziko, mawazo yangu kwa amani kwa sababu mimi hukaa ndani pamoja na Roho wa Mungu mwenyewe! Ananiongoza mimi na kuyifariji roho yangu yenye wasiwasi. Siogope uovu wowote kwa sababu ninalala na kisha kuamuka katika nguvu ya kuokoa ya Roho Mtakatifu - anayeishi ndani yangu! "

"Huku[mkimtwika] yeye fadhaa zenu zote, kwa maana Yeye hujishughulisha sana mambo yenu" (1 Petro 5:7). Ni jambo moja kutaja aya hii na mwingine kuamini! Hebu Roho Mtakatifu ndani yako alete ufunuo wa ukweli wa Neno lake. Atakufunulia siri ya uwepo wake na utakwenda kwa uhuru wa utukufu.

Download PDF