MAHITAJI YA USHILIKIANO WA KIKRISTO | World Challenge

MAHITAJI YA USHILIKIANO WA KIKRISTO

Jim CymbalaAugust 10, 2019

"Wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi yaw engine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia" (Waebrania 10:25).

Ni baraka kufanya ibada pamoja na waumini wengine. Kuimba nyimbo za Bwana, kusikia Neno lake la thamani linafafanuliwa, kuinua sauti zetu kwa sala pamoja na Wakristo wengine, kwa upendo na kupendwa - hizi ni njia ambazo Bwana hutumia kuimarisha mioyo yetu.

Katika siku za Paulo, kuna watu waliokataa ibada ya umma kwa sababu moja au nyingine. Vivyo hivyo, wenzao wa kisasa wana hamu ndogo ya kuwa katika nyumba ya Mungu na watu wake. Hii ni jambo baya, bila kujali mawazo mabaya. Wakati muumini anaanza kuhudhuria kanisa mara kwa mara au mara kwa mara tu, inaweza kuwa ishara ya shida ya kiroho. Kuna maozo mengi mabaya ya kujieleza; "Ninafanya kazi kwa bidii sana nakukalibia kuchoka sana." "Tunahitaji muda zaidi wa familia." "Ninaweza kumwabudu Mungu jikoni mwangu." Au liliyejulikana sana, "Kanisa limejaa wanafiki."

Usiruhusu tamaa au siasa za kanisa zikuzuie kutoka kwa uamsho wa kiroho. Wale ambao hawana hamu ya kuwa pamoja na waumini wengine, kwa kweli, wanahamu kidogo ya Kristo. Kuwa sehemu nzuri ya mwili wa kanisa mara zote inamaanisha mambo mawili: tamaa ya kukaa na uhusiano na unyenyekevu wa kukubali haja yetu kwa waumini wengine. Ikiwa mtume Paulo aliomba sala na alitamani ushirika na waumini, tunapaswa kufanya hivo pia. Sisi wote tunahitaji faraja ya ndugu na dada katika Kristo kutusaidia njiani yetu.

Kuhudhuria kanisa mara kwa mara si suala la uhalali lakini mantiki ya kiroho, hasa kama tunavyoona "Siku" inakaribia. Hivi karibuni Yesu atakuja tena na masuala yote ya maisha yanayotupiga chini yatatoweka katika sekunde chache. Mambo muhimu zaidi ni imani yetu ndani ya Kristo, ukuaji wetu katika neema, matunda tunayozalisha kwa ajili ya utukufu wake, na kutimiza mapenzi yake kwa maisha yetu. Mengi ya maendeleo yetu ya kiroho hutokea tunapozungumza na wajumbe wengine wa mwili wa Kristo mara kwa mara, hivyo kuwa na bidii kukusanyika pamoja na waumini wenzetu.

Jim Cymbala alianzisha Hema la Brooklyn (Brooklyn Tabernacle) akiwa na waumini wasio zidi ishirini katika jengo la chini katikati ya sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.

Download PDF