MASAA YA UDHAIFU MKUBWA ZAIDI | World Challenge

MASAA YA UDHAIFU MKUBWA ZAIDI

Gary WilkersonJuly 22, 2019

"Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, siku zote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema maombi yangu kwa furaha, kwa sababu ya ushirikiano wenu katika kuineza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata hivi sasa. Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi nzuri ndani yenu ataimaliza hata siku ya Yesu Kristo; vile vile kama ilivyo wajibu wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kutetea Injili na kuithisbitisha, ninyi nyote mmeshirikiana name neema hii. Kwa maana Mungu ndiye shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote katika moyo wa upendo wa Kristo Yesu. Na hii diyo ombi langu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; , ili mpate kuyakubali yaliyo mema, na kuwa na mioyo safi, bila hatia mpaka siku ya Kristo; mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu" (Wafilipi 1:3-11).

Mtume Paulo alikuwa ameandikia kanisa la Filipi kutoka jela la Kirumi. Zaidi ya kanisa lolote, waumini hawa walimsaidia katika huduma yake na walikuwa wapenzi sana kwake. Paulo alionyesha upendo wake kwao na shukrani yake kwa ushirikiano wao. Pia, alitaka kuwahamasisha kumtazama Yesu na kumwamini Mungu kukamilisha kazi aliyoanza ndani yao.

Paulo ni mfano mkamilifu wa mtu ambaye huenda kupitia mateso makubwa na anaweka imani yake katika nguvu za Mungu. Zaidi chini tunasoma, "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" (4:13). Paulo alikuwa na uhakika wa uhusiano wake na Yesu na alijua kwamba Mungu angeweza kumsaidia katika masaa yake ya udhaifu mkubwa.

Vivyo hivyo, tuna uhakika kwamba Mungu hutuunga mkono wakati maisha anaonekana kuyumba yumba. Kwamba katika masaa yetu ya udhaifu mkubwa tunayo nguvu ambayo haiwezi kubadilika. Tuna tumaini la kweli-Mungu yu pamoja nasi katika mahitaji yetu.

Unapotembea kupitia majaribio, kuwa na ujasiri kwamba Mungu atakusaidia. Zaidi ya hayo, na kwamba atamaliza ndani yako siku moja kazi aliyoyinza ndani yako. Weka macho yako kwake.

Download PDF