MBELE YA KITI CHA BABA | World Challenge

MBELE YA KITI CHA BABA

David Wilkerson (1931-2011)April 10, 2019

Watumishi wa Mungu wanapaswa kuja mbele yake kikamilifu wakiamini kwamba atajibu. Ni jambo nzuri kuleta ahadi za Mungu katika sala pamoja na wewe – kwa kusimama kama unamkumbusha. Hakika, hapotezi fahamu yakukumbuka, lakini Bwana anatupenda sisi kwa kuleta ahadi zake mbele yake.

Petro alipewa maono na kushangaa  kwa kujiuliza yanaomaanisha. Alipokuwa akitafakari, Mungu akamwambia, "Roho akamwambia, wako watu watatu wanakutafuta. Basi andoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma" (Matendo 10:19-20). Kifungu hiki cha Maandiko kinatuambia kwamba wakati Mungu anatangaza kitu kuwa kweli, tunapaswa kuamini na kusimama juu ya hilo, bila kushauriana na mwili wetu. Hatuwezi kupima kuaminika kwa Neno la Mungu kwa kuchunguza hali yetu au ustahili wetu. Ikiwa tunafanya, tutaishia tu kuona kwamba hatustahili. Kisha tunaweza kuishia kwa kunongoneka wenyewe kinyume nakudai Neno lake na kurifaa.

Biblia inasema sisi ni waombaji katika kiti cha enzi cha Mungu na Kristo yuko pale kama mwombezi wetu au mtetezi wetu. "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu" (1 Timotheo 2:5). "Maana yu hai siku sikuzote ili atuombea [sisi]" (Waebrania 7:25). "Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki" (1 Yohana 2:1).

Kwa damu iliyomwagika ya Yesu msalabani, mlango wa kiti cha Baba uko wazi kwa ajili yetu na tuna uwezo wa kubeba maombi yetu kwa Mungu. Pia tuna Roho Mtakatifu, ambaye ni "msaidizi" wetu, ambaye anasimama kama mshauri wetu, mwalimu, mtetezi, mpatanishi na mwombezi. Anatukumbusha amri za milele na katiba ya Mungu ambavyo vinafanya Neno la Mungu - kwa hiyo tuna ahadi hizi za ajabu.

Ni uhakika kujua kwamba kwa kweli Mungu hufurahia wakati unakaribia kiti chake cha enzi kwa ujasiri, kwa kujifungia kwa Neno lake lenyewe. Naye atahakikisha kwamba unajuwa kama anafurahi pamoja na wewe.

Download PDF