MUNGU ANATAKA KUFANYA YASIOWEZEKANA | World Challenge

MUNGU ANATAKA KUFANYA YASIOWEZEKANA

David Wilkerson (1931-2011)March 14, 2018

Kwa nini Mungu alingojea mpaka Ibrahimu na Sara wawe wazee ili awape mtoto wakiume? Kwa nini alingojea mpaka hali hiyo isiowezekana kwa binadamu na kuwa tu na imani kamili ndani yake ndio ilioweza kuleta ahadi? Ilikuwa ni kwa sababu mbegu hii ilipaswa kuwekwa kabisa katika imani.

Ibrahimu na Sara wote walijua ahadi ya kushangaza ya Mungu kuwapa mtoto wakiume lakini imani yao ilikuwa bado haijawiva. Sara alikosa subira na alipanga mpango, na Ibrahimu alifuata mpango huo. Ishmaeli alizaliwa na wakati ilikuwa ni kweli kuwa alikuwa wa uzao wa Ibrahimu, hakuwa mrithi aliyeahidiwa. Kwa kupotoka kwa asili ya kibinadamu, Sarah alimkasirikia mumewe akiwa na wivu pamoja pia kumlaumu. Wote wawili walikuwa wakijaribu kufanya ahadi ya Mungu kuja na juhudi zao wenyewe (angalia Mwanzo 16:1-15).

Labda unajiuliza kwa nini ahadi yako haijawahi kutekelezwa. Unajaribu kujua jinsi Mungu atakavyokutana na mahitaji yako, na kugeuka yote yenye kujikwaza chini kwa kuzingatia vikwazo badala ya uwezekano.

Ibrahimu na Sara walipewa mtoto wao wa muujiza lakini hawakujuwa kikamilifu kwamba Mungu angetimiza ahadi yake kwa njia yake na wakati wake. Tunajua kwamba waligeuka na kukomaa katika imani yao lakini baada ya kutangatanga - na Ishmael ilikuwa ni ishara ya kupungua kwa imani hio. Baadaye, hata hivyo, alisema juu ya Ibrahimu: "Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi" (Warumi 4:20-21).

Wapendwa, kila kutangatanga munako, hutoka kwa kutokuamini; musijaribu kufikiri mambo au majadiliano maswala ndani yenu. Kuwa na imani inamaanisha kwamba umeweka hoja zako zote na una hakika kabisa kwamba Mungu ataweka Neno lake. Anataka kufanya yasiowezekana kwa sababu hali haiwezekani zaidi, anapata utukufu zaidi!

Download PDF