MUNGU HANA TATIZO KUKUPATA WEWE | World Challenge

MUNGU HANA TATIZO KUKUPATA WEWE

Gary Wilkerson
April 9, 2018

Haijali jinsi giza linakuzunguk au "haujulikani" utambulisho wako, wakati Mungu anachagua kujidhihirisha kwako mwenyewe, hana shida kukupata wewe. Hebu tuangalie mama wa Samson ... mtu mwenye nguvu aliyewahi kuishi.

"Wana wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya BWANA, BWANA akawatia katika mikono ya wafilisti muda wa miaka arobaini. Palikuwa na mtu mmoja wa Sora ... jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, na hakuzaa watoto. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke akamwambia, 'Tazama … nawe utamzaa mtoto mwanamume'" Waamuzi 13:1-3).

Kwa miaka arobaini wana wa Israeli walikuwa wamepotea jangwani, wakawafadhili Wafilisti na wa kaharibiwa kwa roho. Katikati ya machafuko hayo na kukata tamaa aliishi mwanamke mwaminifu, aliyeomba ambaye alimjua Mungu wake. Tunaona kwamba jina la mumewe lilikuwa Manoa lakini mwanamke huyo hakuwa na jina - mtumishi asiyejulikana wa Bwana.

Kama vile kilichotokea katika Agano Jipya na msichana mdogo aitwaye Maria, mke wa Manoah alitembelewa na malaika, ambaye alimpa ujumbe wa kushangaza: "Wewe utabeba mtoto!"

Mke wa Manoa alikuwa mwenye kuwa na subira nyingi wakati wa Israeli walikuwa utumwani, akijifungia mwenyewe katika chumba cha siri na Mungu. Sasa alipokea neno kutoka kwa Bwana. Mtoto wake aliyeahidiwa hakutakiwa kuwa mvulana wa kawaida, kama malaika alivyomwambia kuwa angeenda "kuokoa Israeli kutoka kwa mikono ya Wafilisti" (13:5). Kisha Bwana akatoa maelekezo maalum juu ya jinsi kijana huyo angepaswa kuletwa na kujiandaa kwa wito wake maalum. (Soma akaunti ya kusisimua ya maisha ya Samsoni katika Waamuzi 13 hadi 16.)

Mama wa Samsoni aliamini ahadi za Mungu na akamfundisha mwanaye kulingana na maagizo ya Bwana. Vivyo hivyo, leo Mungu anatafuta watumishi wenye subira, watumishi waliojitolea ambao watamtegemea katika mazingila ya hali kubwa.

Download PDF