MUONGOZO KUTOKA KWA ROHO MTAKATIFU | World Challenge

MUONGOZO KUTOKA KWA ROHO MTAKATIFU

David Wilkerson (1931-2011)December 3, 2019

Kusudi la Mungu kwa watoto wake ni kwamba tunajisalimisha kwa utawala na uzibiti wa Roho Mtakatifu: "Ikiwa tunaishi katika Roho, na tuenende pia katika Roho" (Wagalatia 5:25). Kwa maneno mengine, "Ikiwa anaishi ndani yako, wacha akuongoze!"

Wakristo wa kwanza hawakutembea katika machafuko, kwa sababu waliongozwa na Roho. Waliwasiliana na Roho Mtakatifu na yeye aliwaelekeza. Kutembea katika Roho kunamaanisha uwazi wa kusudi na kutowa uamuzi usio na kiburi.

Tunaona mifano mingi ya kuongozwa na Roho katika Agano Jipya. Mfano mzuri ni Petro: "Wakati [yeye] alifikiria juu ya maono, Roho akamwambia ..." (Matendo10:19). Katika sehemu nyingine, tunasoma, "Roho aliniambia niende pamoja nao, bila shaka yoyote" (11:12). Roho Mtakatifu alitoa mwelekeo na Petro alisikiza.

Kuna faida nyingi za kutembea katika Roho Mtakatifu. Faida moja kwa wale wanaouliza: atakupa mwelekeo, maonyo au chochote unachohitaji. "Lakini Yeye, wakati atapokuja, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza katika ukweli wote" (Yohana 16:13). Yesu hasemi tu juu ya unabii na matukio yajayo hapa, anaongea juu ya maisha yako. Roho Mtakatifu atakuongoza katika mambo ya vitendo sana ya maisha yako ya kila siku.

Kutembea katika Roho pia kunamaanisha kuwa kamwe usishindwe na nguvu za mapepo, hata ingawa Shetani atajaribu kukutisha. Paulo alipambana na unyanyasaji huo kwa nguvu ya Roho: "Ndipo Paulo ... akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu" alipambana na roho mbaya na akashusha nguvu zote za giza (ona Matendo 13:9-11). Inakuja wakati ambapo itakubidi usimame kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na kusema, "Inatosha! Nakuamuru kwa jina la Yesu uende! "

Lakini aina kubwa zaidi ya kutembea katika Roho ni kumruhusu akufundishe mambo ya ndani ya Mungu yaliyofichika. Simama katika uwepo wake na Roho Mtakatifu akuonyeshe moyo wa Bwana. Unapofanya hivi, mwelekeo utakuja na itabidi hata uulize.

Weka moyo wako kumtafuta leo na utajifunza kujua sauti yake. Anza kumsifu, kuimba, kumtegemea Mungu - naye atatunza uokoaji wako.

Download PDF