NGUVU YA KUSHINDA MWILI | World Challenge

NGUVU YA KUSHINDA MWILI

David Wilkerson (1931-2011)August 23, 2019

"Na ile damu itakuwa ishara kwako katika nyumba mtakazokuwamwo; nami nitakapoiona ile dhambi, nitapita juu yenu, ili lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misiri” (Kutoka 12:13).

Usiku wa Pasaka ulikuta familia za Kiyahudi zikifungiwa katika makazi yao, zikingojea kuondoka Misri. Damu ya mwana-kondoo asiye na dowa ilinyunyizwa kwenye kizingiti cha milango ya kila nyumba, kwa amri ya Bwana. Waliahidiwa, "Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi" (12:23). Familia zingine zinaweza kuwa zilikuwa na wasiwasi, wakati zingine zilikuwa zinafurahi, lakini zilikuwa salama kwa usawa chini ya damu.

Ukombozi wa Israeli kutoka Misri ni aina wazi ya ukombozi wetu kutoka kwa dhambi na utumwa wake. "Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya dunia inayo kuja" (1 Wakorintho 10:11). "Kwa maonyo yetu" inamaanisha kuwa tunaweza kuona kwenye mapambano yao kama kivuli cha vita vyetu vya sasa na dhambi na dhambi. Misiri yao ndio ulimwengu wetu usiomcha Mungu.

Waisraeli waliokolewa kutoka kwa nguvu ya Wamisri na mkono wa nguvu wa Mungu. "Kwa maana Bwana alikutoa kutoka Misiri kwa mkono mwenye wuwezo" (Kutoka 13:9). Kama vile damu iliondoa Israeli kutoka kwa hukumu, ndivyo damu ya Yesu inatuokoa na mkono wake wenye nguvu unavunja nguvu ya dhambi ndani yetu. Ndio, dhambi bado inakaa lakini haitawale! Umesamehewa, lakini pia unwo uwezo wa kushinda mwili. Hili ni neno lenye kutia moyo sana katika siku hizi za unyonge.

Kristo anakuja kwa wale wanaomngojea, "Kwa watu pia maliopenda kufunuliwa kwake" (2 Timotheo 4:8). Ni pendeleo gani lisilo la kawaida kama kuwa miongoni mwa wale waliopambwa kama bibi, aliyeoshwa katika damu na kutazamia kuonekana kwake!

Download PDF