SIKILIZA ONYO HILO | World Challenge

SIKILIZA ONYO HILO

David Wilkerson (1931-2011)October 30, 2019

"Kuanzia mdogo wao hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmja nimwenye kuwa na tamaa; na kutoka kwa nabii hata kwa kuhani, kila mtu anatenda uwongo… Je! waliona aibu wakati wamefanya machukizo? Hapana! Hawakuwa na aibu kamwe" (Yeremia 6:13, 15).

Nabii Yeremia aliona hali ya kutisha ikija juu ya watu wa Mungu. Walikuwa wakificha dhambi zao nyuma ya amani na usalama wa hali ya juu. Uchovu ulikuwa umeshinda mioyo yao na maisha yao yote yamekuwa ya juu - machozi ya juu, toba ya juu, hata uponyaji wa juu. Mbaya zaidi ya yote, walikuwa wamepoteza hisia zao za huzuni kwa dhambi - katika jamii, kanisani, katika maisha yao wenyewe. Dhambi ilikuwa "moja tu ya vitu hivyo."

Katika Yeremia 5:1-3, nabii anatupa picha ya kuvunjika kwa maadili ambayo yalitokea katika Israeli na nyumba ya Yuda. Watu wa Mungu walikaa chini ya ujumbe wa ukweli na kweli waliigeuka na kuasi. Hofu yao kwa ajili ya Mungu ilikuwa ikipungua na hapo walipokuwa wamefurahi katika Neno la Mungu, sasa walipuza maonyo ya manabii - walinzi.

Mungu anaweka leo walinzi juu ya kanisa; sauti zenye upako zilizowekwa na Bwana kuwajibika kwa roho yako. Kama mwamini, ni jukumu lako kutii Neno la Mungu na kuwa mtiifu ili uweze kuletwa kwa sura ya kweli ya Kristo. Hiyo inamaanisha kutembea kulingana na ukweli bila kugeuza.

Wakati Mungu hufanya jambo la kweli katika watu wake, Shetani huwa analichunguza kwa ajili ya kulipinga. Wakati Nehemia alipoanza kujenga tena kuta za Yerusalemu, kulikuwa na upinzani mkubwa. "Lakini ikawa kwamba [maadui] waliposikia kwamba kazi ya kujenga kuta za Yerusalemu inaendelea ... walikasirika sana, wakawafanya njama wote kwa pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo" (Nehemia 4:7-8). Vivyo hivyo, mtu anapomgeukia Mungu na kupata kugewuzwa kikamilifu maishani mwake, Shetani atapigana na nguvu zake zote kuzuia maendeleo yake. Weka moyo wako kuwasikiza walinzi na umruhusu Roho Mtakatifu ajaribu moyo wako kwa undani ili uweze kutembea kikamilifu mbele ya Bwana katika saa hii ya mwisho.

Download PDF