TUMIKIA MAHALI ULIPOPANDWA | World Challenge

TUMIKIA MAHALI ULIPOPANDWA

Carter ConlonNovember 9, 2019

"Alipopaa juu, aliteka mateka, na akawapa wanadamu vipawa" (Waefeso 4:8).

Yesu alichukua mateka, ambayo inamaanisha kwamba vizuizi vya zamani kwenye maisha yako - sauti ambazo zimekuambia kuwa wewe sio mtu wa kutosha au mwenye talanta ya kutosha, maneno mabaya ambayo yamezungumzwa juu yako - yote yameenda. Sasa wewe ni kiumbe kipya katika Kristo na unayo mwito wa kipekee.

Mwito huu wa kipekee kwa kila mmoja kuhusu maisha yetu, hautaweza kutufikisha mahali ambapo hatuna nguvu ya kawaida ya kwenda ili Kristo apate kutukuzwa kupitia hayo yote. Ndio maana “alitoa vipawa kwa wanadamu.” Kwa maneno mengine, kila mmoja hupewa kile tunachohitaji ili kutimiza kusudi lake katika maisha yetu.

Kama mchungaji kijana huko Canada, nilikuwa nimeazimia kushinda ulimwengu wote kwa Kristo! Nilianza na shauku ya kufanya kile nilichohisi kuwa ninatakiwa kufanya, kilikuwa ni kufunga, kuomba, na kusafiri sana ili kuhudumu. Kwa kufanya hivyo, nilijaza kabisa nguvu yangu ya mwili wakati nilikuwa na umri wa miaka thelathini na saba. Kwa kweli Mungu kwa upendo wake alinionyesha kuwa wakati nitasimama mbele yake siku moja, hakutakuwa na thawabu kwa mambo ambayo hakuniuliza nifanye. Alinitaka niwajibike kwa mkutano mdogo ambao nilikabidhiwa - wote mia moja na hamsini na wanane kati yao. Aliweka hilo wazi kwangu kwamba kutembea kwao na Mungu ndio jukumu langu kuu. Siku hiyo nilitangaza, "Bwana, kwa maisha yangu yote nitakutumikia ukinipanda na sitaangalia zaidi ya kile ulichonipa kufanya." Furaha kubwa iliniingia moyoni na nguvu yangu ya mwili ikaanza kurudi.

Kumbuka, Mungu amekuweka kimpango mahali ulipo. Sio lazima kuwa mkubwa machoni pa wanadamu. Mtumikie vema tu na umwamini kila siku ili neema atimize kusudi lake lote kwa maisha yako - hadi wakati huo huo utakaposimama mbele ya kiti chake cha enzi, na kumsikia akisema, “Ulifanya kanzi nzuri, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache, nitakufanya uwe mtawala wa vitu vingi. Ingia katika furaha ya Bwana wako!” (Ona Mathayo 25:23).

Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa Kanisa la Times Square mnamo 1994 katika mwaliko wa mchungaji mwanzilishi, David Wilkerson, na aliteuliwa kuwa Mchungaji Mwandamizi mnamo 2001.

Download PDF