UJASIRI WA KUKABILIANA NA ADUI | World Challenge

UJASIRI WA KUKABILIANA NA ADUI

Carter ConlonDecember 7, 2019

Yesu aliwahi kusema, "mwizi haji ila kuiba, na kuua, na kuharibu. Nimekuja ili wawe na uzima, na kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10).

Wewe na mimi pia tunakabiliwa na mwizi leo - mtu ambaye amekuja kuiba mustakabali wetu, familia zetu, furaha yetu, tumaini letu, na ufanisi wetu duniani. Lakini, Yesu anatukumbusha kwamba ametengeneza njia ya kuwa na maisha tele. Na kwa hivyo lazima tuelewe kwamba tuna nguvu ya kumshinda adui.

Shetani atajaribu kukushawishi kwamba ushindi hauwezekani. Lakini, yeye ni mwongo! Mungu amekuita, na pia kukupatia vifaa vya kumshinda shetani. Daudi mtunga-Zaburi alisema hivi hivi: “Maana kwa msaada wako na weza kukimbia kundi la jeshi. Kwa msaada Mungu wangu naweza kuruka juu ya ukuta… kwa maana umenitia nguvu kwa vita” (Zaburi 18:29, 39).

Paulo anatufundisha katika kitabu cha Waefeso: "Mwishowe, ndugu zangu, kuwa wenye nguvu katika Bwana na kwa uweza wa nguvu Zake. Vaa silaha zote za Mungu, ili uweze kusimama dhidi ya ujanja wa ibilisi” (Waefeso 6:10-11). Kwa maneno mengine, "Kuwa na nguvu ndani ya moyo wako. Tembea katika uhusiano mzuri na Mungu. "Ninakuhimiza ujue Biblia yako, kwa kuwa ni silaha yako!

Haupigani na adui peke yako. Muombe Bwana akupe maono ya wewe ni nani ndani ya Kristo, maono ya kwanini "hata pepo huamini-na kutetemeka" (Yakobo 2:19). Nabii Elisha aliwahi kuomba jambo kama hilo ili kumtia moyo mtumwa wake mwenye woga. “Usiogope, kwa maana wale walio pamoja nasi ni zaidi ya wale walio pamoja nao.”

Usitetemeke wakati unakabiliwa na adui! Una silaha za Kristo, ushirika wa kaka na dada ambao wapo ili kusaidia, na Yesu, Genelo Mkuu. Hauko peke yako!

Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa Kanisa la Times Square mnamo 1994 katika mwaliko wa mchungaji mwanzilishi, David Wilkerson, na aliteuliwa kuwa Mchungaji Mwandamizi mnamo 2001.

Download PDF