UKUU WA MUNGU WETU | World Challenge

UKUU WA MUNGU WETU

David Wilkerson (1931-2011)November 24, 2017

Mtunga Zaburi Daudi anatukumbusha ukuu wa Mungu hata kati kati ya mafuriko makubwa. Maji yetu ya sasa yanaweza kuinua sauti yake kwa sauti kubwa, lakini Mungu anatawala juu ya kila kitu. Yeye peke yake yuko katika udhibiti.

Sauti za Daudi ni malalamiko ya wale waliojaa hofu za mafuriko nda ya nafsi zao: "Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Ninazama katika matope mengi, pasipowezekana kusimama. Nimefika kwenye maji ya vilindi, mkondo wa maji unanigharikisha. Nimechoka kwa kulia kwangu, koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofukwa kumngoja Mungu wangu" (Zaburi 69:1-3).

Ndio, Daudi pia ametupa jibu latu kati la kila mafuriko makubwa: "Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana aliye juu ndiye mwenye ukuu" (93:4).

Hivi sasa, maji ya gharika yanaongezeka kwa waamini wengi - mateso, majaribio, matatizo magumu, wasiwasi juu ya matukio ya ulimwengu. Lakini Mungu ametangaza ahadi hii: "Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakughalrikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza" (Isaya 43:2).

"Bwana amejaa huruma na neema, haoni haoni hasira upesi, ni mwingi wa wa fadhili. . . . Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, kadiri ile ile reheme zake ni kuu kwa wamchao. . . . Bali fadhili za Bwana zina wamchao tangu milele hata milele, na haki yake ina wana wa wana" (Zaburi 103:8, 11, 17).

"Maana fadhili zako nikubwa hata mbinguni. . . . Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako" (108:4-5).

"Bali mimi ni kama mzeituni umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele" (52:8).

Ruhusu Neno la Mungu likuangazie na likuimarishe katika yote unayofanya! 

Download PDF