UNAFANYA NINI UNAPOFADHAIKA? | World Challenge

UNAFANYA NINI UNAPOFADHAIKA?

David Wilkerson (1931-2011)
June 13, 2018

Somo la kutoa shukrani likanijia wakati wa uzito mkubwa wa kibinafsi. Matatizo mengi yalikuwa yameongezeka kwa kuwa mimi nilikuwa nimefanya kitu bila kufikilia kwa mke wangu, "Nimekuwa nakaribia hilo. Mimi niko kwenye mwisho wa kamba yangu na ninataka tu kutoweka!"

Kuhisi huruma sana kwangu, nilianza kulalamikia Mungu, "Bwana, ni muda gani utanaweka katika moto huu? Je, huoni jinsi shida yangu imekuwa? Unataka kujibu wakati gani, eeh Mungu?"

Ghafla Roho Mtakatifu akatua juu yangu na niliona aibu. Alinung'unika kwa moyo wangu, "Anza tu kunishukuru hivi sasa, Daudi. Leta kwangu dhabihu ya shukrani kwa yale yote niliyokufanyia zamani na kwa yale ninaenda kutenda baadaye.

Towa shukrani kwangu kuhusu familia yako, afya yako, huduma yako. Nipe tu sadaka ya shukrani na kila kitu kitaonekana tofauti. Utakuwa na amani katika vita na nitabariki nafsi yako kwa uhakika."

Maneno hayo yaliimarisha roho yangu lakini nilijiuliza nini Bwana alimaanisha kwa "dhabihu ya shukrani." Kutafuta Neno, nilishangaa kwa marejeo yote niliyoyaona.

"Na wamtolee dhabibu za kushukuru, na kuyasimulia matendo yake kwa furaha" (Zaburi 107:22).

"Nitakutolea dhabibu ya kushukuru; na kulitangaza jina la Bwana" (Zaburi 116:17) "Tuje mbele zake kwa shukrani, tumufanyie shangwe kwa Zaburi" (Zaburi 95:2). Na kwa kweli, sehemu ya Biblia inayojulikana juu ya shukrani: "Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, Nyuani mwake kwa  kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake" (Zaburi 100:4).

Wakati hauna nafasi ya kugeuka, geukia kwa kutoa shukrani! Towa shukrani kwa Bwana kuhusu msamaha wake, baraka zake, ahadi zake, yote aliyo yafanya na atafanya. Katika kila kitu, towa shukrani!

Download PDF