UNAKARIBIA KUWA HURU! | World Challenge

UNAKARIBIA KUWA HURU!

David Wilkerson (1931-2011)April 5, 2018

Biblia inaonyesha wazi kwamba nguvu za pepo ziko kwenye kazi kwa kuweka mitego kwa Wakristo. Shetani ameamua kabisa kuharibu kila mwamini anayeenda katika utakatifu na kujitolea kamili kwa Yesu Kristo. Sasa elewa, Shetani haupo popote - hawezi kuwa popote mara moja - na hajui mambo yote. Lakini anacho kama amri yake kwa mapepo mengi, mamlaka na nguvu za giza. Na nguvu hizi za giza zinaweka mitego kwa ajili yako. "Watendao uovu wamenitegea mtego" (Zaburi 119:110). "Katika njia niendayo wamenifichia mtego" (Zaburi 142:3).

Mpendwa, shetani anaweka mtego kwako usioweza kuona. Kwa hiyo, lazima uwe muangalifu wakati wote. Anaweza kutumia watu waovu, anaweza kutumia majaribu ya mwili, au anaweza hata kutumia Wakristo wengine, lakini unaweza kuwa na uhakika kama Shetani yuko nyuma ku kutega ili uingie katika dhambi.

Ikiwa umekuwa mutekwa alio anguka katika mtego wake na sasa unaishi katika utumwa, lazima uelewe kuanguka kwako kwa uwezekano mkubwa sio uliofikiliwa mbele. Ibilisi alijua udhaifu ndani yako na akakusumbua kimawazo kupitia hilo. Unaweza kuendelea kujilaumu, kwakufikiri, "Ningewezaje kufanya kitu kama hicho?" Lakini kujipiga mwenyewe ni kupoteza muda kabisa! Huwezi kamwe kujua jinsi ungeweza kuwa mjinga, kipofu na mwenyekutokua na wasiwasi, basi fikiria akili yako juu ya Yesu kwa sababu nina habari njema kwako. Wewe unakaribia kuwa huru!

Ikiwa umefungwa na adui kwa njia yoyote na kuanguka katika mtego wake, lakini unajua unampenda Mungu kwa moyo wako wote, Bwana hatakuacha wewe uendeleye kuwa muasiliwa wa adui. Soma Neno la Mungu kwa kujitolea upya na kumwomba Roho Mtakatifu akupe ufahamu wa kuchaguwa yalio mema. Kuna nguvu kwa jina la Yesu na atakuokoa na atakulinda!

Download PDF