WATENDAJI WA ROHO MTAKATIFU | World Challenge

WATENDAJI WA ROHO MTAKATIFU

David Wilkerson (1931-2011)September 20, 2019

Kanisa la leo limejaa watakatifu wenye kimya ambao hawataki kufanya mawimbi. Baada ya yote, hakuna mtu anayetaka shida! Lakini baadhi ya wanafunzi walikuwa wasumbuwaji wakuu. Paulo na Sila walitembea kwa nguvu ya Roho na "wakatoa maisha yao kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo" (Matendo 15:26). Katika kipindi kimoja, Paulo aligongana na muuzaji wa bahati ya kunena, na kutowa roho mbaya ndani yake, na kupelekea mji wote kufanya ghasia. Wamiliki wa mtumwa wa yule mama aliyeokolewa walivuta Paul na Sila ndani ya soko ili kusimama mbele ya mahakimu wa jiji. Kisha wakawapiga na kuwatupa gerezani (ona Matendo 16:16-24).

Kwa kweli inaonekana kwamba Shetani alikuwa ameshinda vita hii, lakini nguvu zote za Mungu zilikuwa na hawa watendaji wa Roho Mtakatifu. "Usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za Mungu ... [na] ghafla kulitokea mtetemeko mkubwa wa ardhi, hata misingi ya gereza ikatikisika; na mara moja milango yote ikafunguliwa, na minyororo ya kila mtu ikafunguliwa.” (16:25-26). Matokeo moja ya yote ni kwamba mchunga gereza alianguka chini mbele ya wale watu na kulia, "Mabwana, nifanye nini ili niokole?" (16:30). Baada ya kutoka gerezani, Paulo na Sila walienda moja kwa moja nyumbani kwa Lidia na kuwatia moyo ndugu zao katika Bwana (ona 16:40).

Paulo na Sila walipigana bila woga nguvu za giza na mfumo mbaya wa kidini. "Walifika Thesalonike, ambapo kulikuwa na sinagogi la Wayahudi. Ndipo Paulo… akajadiliana nao kutoka kwa maandiko, akafafanua na kuonyesha kuwa Kristo alilazimika kuteseka na kufufuka kutoka kwa wafu, na kusema, 'Yesu huyu ninayemhubiri yeye ni Kristo'” (17:1-3). Sinagogi kule Thesalonike labda lilikuwa limefanya mikutano ya utulivu kwa miaka, bila shida. Walifundisha Maandiko kwa bidii na kwa nje walionekana watakatifu sana. Ndipo Paulo alifika na katika majuma matatu tu ya kuhubiri ufalme wa Yesu, akageuza eneo lote hilo.

Je! Umewahi kutamani kuwa na bidii zaidi katika ushuhuda wako? Je! Shetani amekufanya uwogope wanadamu? Bibilia inasema, "Mpegeni shetani naye atawakimbia" (Yakobo 4:7). "Hatimaye ndugu zangu, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake" (Waefeso 6:10). Acha Paulo na Sila wakuhimize kuwa jasiri katika ushuhuda wako kwa ajili ya Yesu.

Download PDF