WAUMINI WA KWELI WANAOSHIKILIA | World Challenge

WAUMINI WA KWELI WANAOSHIKILIA

David Wilkerson (1931-2011)September 12, 2019

Kanisa la Agano Jipya lilizaliwa katika mwangaza wa utukufu. Roho Mtakatifu alishuka juu yake akiwa kama moto, na Wakristo wa kwanza walizungumza kwa lugha na kutabiri. Hofu ya Mungu ikawaangukia na wale wote waliowaona, na umati ukageuzwa. Lilikuwa kanisa la ushindi, haliogopi Shetani, lisilotowa heshimu kwa sanamu, lisilo tetemeshwa na mapigo au mateso. Lilikuwa kanisa lililosafishwa na damu, hai na kufa kwa ushindi.

Je! Kanisa litatokaje katika saa yake ya mwisho? Je! Litatoka kama kanisa lenye mafuta, lenye mafanikio, ni kanisa la kujipenda lenyewe? Je! Litakuwa kanisa la watu wachache tu lenye waumini wakweli walio shikilia, kwakutazama kifo na uasi ukila kama saratani? Je! Kanisa la siku za mwisho litakaa kwa hofu na woga kwani kwa sababu wachache ndio walioshinda ulimwengu?

Ili kuwa na hakika, kutakuwa na kuanguka mbali; kutakuwa na wadanganyifu wa kufundisha mafundisho ya mapepo na hata wateule wengine watajaribiwa sana. Lakini kanisa la Yesu Kristo haliendi na mtu yeyote anaenungunika. Inatoka mshindi, kwa furaha isiyoweza kusikika, ikipanda mto wa amani. Linakwenda nje kwa ajili ya ushindi, na kila mshiriki wa kanisa hili la kweli ataishi na kufa bila woga. Waumini wa siku za mwisho watakuwa wenye nguvu sana katika Bwana kama Wakristo wa kwanza!

Kanisa litaenda kupitia kutojikimiza kwa kueneza upendo, huruma, na fadhili zisizostahiliwa. Itakuja wakati wa shida kubwa, na wasiwasi juu ya pande zote. "'Kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako ...' Fadhili zangu hazitatoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa, asema BWANA, aliye na huruma kwako" (Isaya 54:8-10).

Mungu atakuwa na watu wanaoshinda. Baba mwenye rehema atawavutia watoto wake kwake na kukomboa umati ambao ulimgeukia. Anachosema kwa kanisa hilo anasema pia kwa waumini mmoja mmoja. Ni wewe? Unapitiya usumbufu wa ghafla na mkali? Ahadi ya Mungu ni kwa wote ambao wametupwa katika dhoruba. Ameamua kufunga nyakati kwa utukuzaji mkubwa wa jina lake. Ni onyesho gani la ajabu ambalo litakuwa!

Download PDF