​MUNGU AMESHIKILIA NENO LAKE

David Wilkerson (1931-2011)

Ujasiri katika sala hutoka kwa kuwa na ujuzi wa kitu kinachoitwa "kushikilia kipaumbele." Ikiwa unaweza kuelewa ukweli huu, utabadili milele namna yakuomba. Mfano ni "kesi iliyotangulia" ambayo hutumika kama mfano katika kesi zifuatazo. Na "kushikilia kipaumbele" ni uamuzi wa kisheria uliofanywa zamani ambao unakuwa utawala wa mamlaka kwa kesi sawa za baadaye. Kwa majaji, hii inamaanisha kusimamia uamuzi uliofanywa tayari.

Wanasheria wazuri wanategemea mara kwa mara "shikilia kipaombele" kwa kesi zao kwa sababu wanajua kipaombele kitasimama mahakamani. Wanatafuta vitabu vyao vya sheria ili kupata kesi nzuri kutoka tangu zamani ambazo zinaweza kuimarisha hoja zao mahakamani, na pia wanatafuta sana mashauri kutoka kwa washauri wa kisheria wenye ujuzi ambao wanaonyesha kipaombele cha awali ili kuzingatia kesi yao wenyewe.

Kwa njia ya Biblia tunapata wanaume na wanawake watakatifu wanaotafuta aina hii ya "kushikilia kipaumbele." Mfano kamili wa hili ni Mfalme Yehoshafati. Yehoshafati alipotawala Yuda, alikuwa na jeshi lenye uvamizi. Taifa hilo lilitetemekaa kwa kutokuwa na msada mbele ya nguvu hii kubwa, kwa hiyo Yehoshafati "akajitahidi kumtafuta Bwana, akatangaza toba katika Yuda yote" (2 Mambo ya Nyakati 20:3). Watu waliomba, walifunga, wakiombewa na kutubu - na mfalme akaleta "Kipaombele cha huruma za Mungu" mbele yake:

"Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si Wewe ulieye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye  juu ya falme zote za mataifa? Wala mkononi mwako hamna nguvu na uwezo, hata mtu asiweze kusimama mbele yako?" (20:6). Yehoshafati anashikilia Mungu kwa huruma zake za zamani: "Si we, Ee Mungu wetu uliewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, na ukulipatia wazao wa Ibrahimu rafiki yako wa milele?" (20:7).

Yehoshafati alimkumbusha Mungu, "Bwana, uliwapa watu wako neno la milele, na ninalileta mbele yako sasa. Ahadi ulizozifanya kwa Ibrahimu na baba zetu bado unaendelea kuzishikilia ili uzitimize. "Bila shaka, Mungu alijibu Yehoshafati, na adui wa Yuda alishindwa. Mungu alikuwa ameshikilia Neno lake mwenyewe.

Kuwa na ujasiri katika sala leo na umuangalie ili atimize ahadi zake katika maisha yako.