JIHIMIZE MWENYEWE KATIKA BWANA

David Wilkerson (1931-2011)

Wengine wanafikiria kuwa waumini wanapaswa kuwa na uhakika kwa kila wakati, kila wakati wakiwa na uhakika wa wapi wanapokwenda, kila wakati kujazwa wenyewe na kuridhika, lakini mara nyingi hisia zetu hufurahi maumivu, mkanganyiko na huzuni. Wanaume na wanawake wote wa kweli wa Mungu wamepata mambo kama haya. Ikiwa unajisikia kufilisika kiroho, kimwili na kimiwazo, ukijua kuwa bila kuingizwa kwa nguvu ya Kristo huwezi kuendelea, hauko peke yako. Lakini kuwa na uhakika kwamba kuna ushindi kamili kwa ajili yako!

Bibilia imejaa akaunti za watu wakubwa wa Mungu ambao walimalizia kwa kamba yao. Daudi ni mfano wa "mtu anayeupendeza moyo wa Mungu" (Matendo 13:22) na wakati mwingine alikuwa amejawa na huzuni, unyogovu, na hisia mbaya za kila aina. "Nimechanganikiwa, nimepindika na kuinama sana, Ninaomboleza siku nzima” (Zaburi 38:6).

Je! Ni kwanini Daudi aliruhusiwa kuvumilia upotevu mwingi na msukosuko katika maisha yake? Baadhi yake ilikuja kama matokeo ya dhambi yake, ambayo yeye alitubu kwa huzuni, lakini pia ni kwa sababu tabia ya Uungu ilikuwa inajengwa ndani yake. Hakuna wakati Roho Mtakatifu hakuwa na Daudi, lakini aliruhusiwa kumaliza mwenyewe wakati mwingine.

Mungu anaahidi nguvu kwa watiwa-mafuta wake: “Abarikiwe Bwana, kwa sababu Amesikia sauti ya ombi langu! Bwana ndiye nguvu yangu na ngao yangu… moyo wangu unafurahi sana na kwa wimbo wangu nitamsifu” (Zaburi 28:6-7). Ikiwa utamwita, atamwaga nguvu zake ndani yako: “Siku ile niliyokuita uliniitikia, na ukafariji nafsi yangu kwa kutiya nguvu roho yangu… Ninatembea kwa kupitiya shida, Utaninyosha; Utanyosha mkono wako… na mkono wako wa kulia utaniokoa” (Zaburi 138:3, 7).

Unaweza kumwamini Bwana kukuona kupitia hali yoyote katika maisha yako. Neno la Mungu limejaa ahadi tukufu na Bwana anafurahia  imani na uwaminifu wetu. Usijali kujihimiza mwenyewe katika Bwana, kama vile Daud alivyofanya, na kukuwa kwa nguvu na kuwa na nguvu zaidi kila siku.