Ameyapaka Macho Yao Ndiposa Wasiweze Kuona | World Challenge

Ameyapaka Macho Yao Ndiposa Wasiweze Kuona

David WilkersonSeptember 18, 1985

“Wote wachongao sanamu ni ubatili, vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wangesema juu yao ni vipofu, ni wajinga, ili wao waaibike. Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu, ambayo haiwezi kumfaidia kitu cho chote? Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa, mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu. Wote na wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao, atashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha. Muhunzi huchukua kifaa na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto, hutengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake. Huona njaa na kupoteza nguvu zake, asipokunywa maji huzimia. Seremala hupima kwa kutumia kamba na huuchora mstari kwa kalamu, huchonga kwa patasi na kutia alama kwa bikari, huifanyiza katika mbo la binadamu, la mwanadamu katika utukufu wake wote, ili iweze kukaa kwenye sanduku lenye vitu vyake vya ibada. Hukata miti ya mierezi, huchukua mteashuri au mwaloni. Huuacha ukue miongoni mwa miti ya au hupanda msonobari, mvua huufanya ukue. Ni kuni kwa ajili ya binadamu, huchukua baadhi yake na kuota moto, huwasha moto na kuoka mkate. Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu, huitengeneza sanamu na kuisujudia. Sehemu ya kuni huziweka motoni, akapikia chakula chake, hubanika nyama na kula hadi ashibe. Huota moto na kusema, ‘‘Aha! ninahisi joto, ninaona moto.’’ Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake, huisujudia na kuiabudu. Huiomba na kusema, ‘‘Niokoe, wewe ni mungu wangu.’’ Hawajui cho chote, hawaelewi cho chote, macho yao yamefungwa hivyo hawawezi kuona, akili zao zimefungwa hivyo hawawezi kufahamu. Wala hakuna anayefikiri, hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema, “Sehemu yake nilitumia kwa kuni, hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake, nilibanika nyama na kuila. Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki? Je, nisujudie gogo la mti?’’ Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha, hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema, “Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si uongo?’’ (Isaya 44:9-20).

Umekwisha soma hadithi hii ilio katika neno la Mungu kuhusu Upofu wa ajabu mno. Hapa tunamuona mwana wa Israeli aliye anguka kutoka kwa Imani, akataye mti, kisha ywaweka kipande kimoja kwa moto kupikia chakula, na kipande kingine akichonga kama sanamu kisha anakiita mungu! Itakuwa aje kwamba manadamu mwenye hekima awe kipofu kiasi hicho, asiye jua lolote na akosaye kipawa cha Uangaji. Ni kwa sababu ya lile Mwenyezi Mungu alilomfanyia mtu huyu. Mungu aliyapaka macho yake asiweze kuona wala kuangaza lolote. Mtu huyu amekula Jivu, macho yake hayaoni, na moyo wake ulidanganyika. Anaishi katika uongo; haoni umuhimu wa usaidizi wala ukombozi; kwa sababu hana habari kamwe ya jinsi hali yake inavyo sikitisha mno. Tuna mtazama mtu huyu asiye na akili na tunanakili Upofu wa ajabu mno. Walakini, Mungu asema hakuna aliye kipofu kuliko watumishi wake! ‘‘Sikieni, enyi viziwi, tazameni, enyi vipofu mpate kuona! Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu, aliye kipofu kama mtumishi wa BWANA? Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia, masikio yenu yako wazi lakini hamsikii cho chote.’’ Ilimpendeza BWANA kwa ajili ya haki yake kufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu. Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara, wote wamenaswa katika mashimo, au wamefichwa katika magereza, wamekuwa nyara, wala hapana ye yote awaokoaye, wamefanywa mateka, wala hapana ye yote asemaye “Warudishe.” Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao? Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, na Israeli kwa wateka nyara? Je hakuwa BWANA, ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake. Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka, ukali wa vita. Ikawazunguka kwa miali ya moto, hata hivyo hawakuelewa, ikawateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.” (Isaya 42:18-25).

Isaya amulika hali ya kanisa la Mungu katika nyakati hizi za Leo. Ni kana kwamba hakuna tena karama ya Uangaji! Msikilize Nabii wa Mungu tena: “Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu, aliye kipofu kama mtumishi wa BWANA?” Nabii asema, “Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia, masikio yenu yako wazi lakini hamsikii cho chote. (munabadilisha vikao vya Semina, mwasoma vitabu bila kukoma, lakini maisha yenu hayageuka kulingana na Utakatifu wa mungu). Watu wa Mungu wanaporwa na kunyang’anywa na mawimbi ya nguvu ya Mafundisho mapya. Mafundisho ya mapepo yamewafunga wengi katika jela za upotevu wa matumaini. Wakristo wapya wamekuwa chakula cha Mafundisho haya ya aibu, na wamegeuzwa kuwa Mavuno kwa Shetani. Kumebaki Watumushi wachache sana wenye karama ya Uangaji, kuona yale yasio na utakatifu wa Mungu, wale wawezao kusema, Imetosha! Hii ni Makosa makubwa mno. Watumishi wachache sana wanaolia, “Warudishie yalio yao!”, wachache sana walio na ufahamu wa kiungu na kuelewa kwa undani wawezao kukomboa walio danganywa na walio fungwa pingu za ibilisi. Upofu huu katika Watumishi wa Mungu umetoka wapi? Imetokana na DHAMBI katika nyoyo za Wachungaji na waumini inayo sababisha ukame wa karama ya Uangaji katika Nyumba ya Bwana. Isaya asema, “Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake”. Johana anatabiri kuhusu kanisa la nyakati za mwisho la Laodikia ambalo ni Kipofu bila kujua: “Kwa maana unasema, ‘Mimi ni tajiri, nimefanikiwa, wala sihitaji kitu cho chote.’ Hujui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, masikini, kipofu, tena uliye uchi” (Ufunuo 3:17).

Dunia inagusa na kuchafua karibu kila kitu katika nyumba ya Bwana na watu wachache sana wameshutuliwa na jambo hili. Kwanini? Isaya alisema, “Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka, ukali wa vita. Ikawazunguka kwa miali ya moto, hata hivyo hawakuelewa, ikawateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.” (Isaya 42:25). Tumekuwa na tabia ya kupeana sababu ya dhambi na kukubaliana na dhambi. Densi za aibu zimeingia kanisani polepole sasa waumini wamefikishwa disko! zinazo andaliwa na Kanisa usiku! Katika Upofu Kanisa linaendelea kuporomoka likielekea kurudi duniani. Tamaa ya ngono inakuzwa haswa kwa madhabahu ya Bwana. Kucheza kanisani kulingana na muelekezo wa Roho Mtakatifu kumsifu Bwana Yesu kwa vifijo na nderemo ni sawa, lakini densi zilizopangwa Kidunia zilizo na aibu na zinazo ubiri ngono zinaonyesha tu mwongozo wa kimwili. Kwa kweli, maelfu ya Watumishi na Wachungaji wamenunua Televisheni zinazoweza kunasa vipindi vya ngono kutoka kwa mtandao. Watu wa Mungu wengi sasa wanasimama kwa Madhabahu wakiubiri Utakatifu wa Mungu alafu wanarudi kukaa ndani ya sanamu za Shetani wakiburudika na filamu za ngono. Nani awezaye kutafakari kwamba Shetani anatumia hizi silaha kuiba Imani ya waumini, kuharibu Amani yao, kuchafua Utakatifu wao, kuvunja Nyumba zao na kuangusha Watumishi wa Mungu? Wako wapi Wachungaji wanao lia, “Turudishieni nyumba zetu zilizo simama imara!, Turudishieni Nyumba zetu zisizo na sanamu, vita na uchafu wa ngono!”.

Wakristo wengi siku hizi ni walevi, wanenda disko na wanapenda kusherekea mambo ya kidunia. Alafu unawaona kwa Nyumba ya Bwana na mikono juu wakisifu na kupiga makofi! Wakiimba Hosanna! Jameni ni sauti nzuri namna gani wanayo inua kwa Bwana? Lakini hawawezi kutambua mema na Mabaya, mambo ya Kiroho na mambo ya Kimwili. Isaya atoa Onyo: “Ole wao wanaoita ubaya ni wema na wema ni ubaya, wawekao giza badala ya nuru na nuru badala ya giza, wawekao uchungu badala ya utamu na utamu badala ya uchungu”.(Isaya 5:20). Inasikitisha sana kwamba kuna wachungaji wachache wanao tambua mambo haya, wanaoweza kuwaita waumini kutoka kwa tamaa zao za kidunia. Inasikitisha tena zaidi kwamba Wakristo wengi wanao muhofu Mungu wataanguka dhambini, watapotea tu kwa sababu ya kukosa kipawa cha Uangaji. Itakuwa ngumu kuepuka nyakati za kishetani ambazo zinaendelea kuongezeka kwa sasa. Neno la Mungu linasema: “Mwenye haki hupotea, wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake, watu watauwa huondolewa, wala hakuna hata mmoja anayeelewa kuwa wenye haki wameondolewa wasipatikane na maovu. (Isaya 57:1). Kwanini Wakristo wengi walio wa kweli wanadanganyika na mafundisho yaubinafsi, yanayo ubiria mwili wala si Roho? Ni kwa sababu hakuna anaye elewa wala anaye tambua. Ni mfano wa uungu usiyo na nguvu kamwe, uliyo na utakatifu mchache mno. “Jambo la kutisha na kushtusha limetokea katika nchi hii: Manabii wanatabiri uongo, makuhani wanatawala kwa mamlaka yao wenyewe, nao watu wangu wanapenda hivyo. Lakini mtafanya nini mwisho wake?” (Yeremia 5: 30-31).

“miungu ya nyakati mypa” ni mfano wa filamu ya kusikitisha sana na ya kuvunja moyo inayo onyesha vile vijana wa siku hizi wamevutiwa na wameuza akili na mitima yao kwa maguru wa Kiindi. Nimestaajabishwa na ukosefu wa karama ya Uangaji katika vijana wetu wa nchi hii (Merikani – lakini hata kwa Nchi zingine pia). Inaweza kuwa kwamba haya ni matokea tu ya ukosefu wa Uangaji na Upofu uliyo Kanisani? Isaya alisema: “Walinzi wa Israeli ni vipofu, wote wamepungukiwa na maarifa, wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kubweka, hulala na kuota, hupenda kulala. Ni mbwa wenye tamaa kubwa, kamwe hawatosheki. Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu, wote wamegeukia njia yao wenyewe, kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe”. (Isaya 56: 10-11). Hali hii ya kukosa Uangaji katika watu wa Mungu lilikuwa pia jambo lilomsumbua moyo Yeremia. Upofu wa Israeli ulimshinda kuelewa na akalia: “Ee mtima wangu, mtima wangu! Ninagaagaa kwa maumivu. Ee maumivu makuu ya moyo wangu! Moyo wangu umefadhaika ndani yangu, siwezi kunyamaza. Kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta, nimesikia kelele ya vita. Maafa baada ya maafa, nchi yote imekuwa magofu. Kwa ghafula mahema yangu yameangamizwa, makazi yangu kwa muda mfupi. Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita na kusikia sauti za tarumbeta? “Watu wangu ni wapumbavu, hawanijui mimi. Ni watoto wasio na akili, hawana ufahamu. Ni hodari kutenda mabaya, hawajui kutenda yaliyo mema”. (Yeremia 4:19-22).

“katika ukahaba, divai ya zamani na divai mpya, ambavyo huondoa ufahamu 12wa watu wangu. Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti nao hujibiwa na fimbo ya mti. Roho ya ukahaba imewapotosha, hawana uaminifu kwa Mungu wao”. (Hosea 4:11-12). Soma tena: “Roho ya ukahaba imewapotosha, hawana uaminifu kwa Mungu wao”. Mtu wa Mungu mwenye dhambi ya kisiri, mtu anayejiingiza kwa dhambi kila mara, mkristo anaye ishi kimwili, atapoteza kipawa cha Uangaji na kuelewa mambo ya kiroho, macho yeke yata pakwa na kuzibwa! Yeye ni kipofu, amepokonywa hekima zote za kiroho na ufahamu wote wa kiroho. “Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao na ugumu wa mioyo yao. Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi”. (Waefeso 4:17-19). Wamekuwa na roho ngumu, wameleweshwa na dhambi, wamejipeana kuishi kimwili wakiyatenda mambo yote ya uchafu wakiwa na tamaa chungu nzima! Timotheo yaonya kwamba: “Roho asema waziwazi kwamba katika siku za mwisho baadhi ya watu wataiacha imani na kufuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. 2Mafundisho kama hayo huja kwa kupitia kwa waongo ambao ni wanafiki hali dhamiri zao zikiungua kwa kuchomwa na moto”. (1 Tim 4:1-2). Baadhi ya watu hawa watakuwa watu wa Mungu waliodanganywa na roho za uongo na mafundisho ya mapepo ya kuzimu. Watumishi wa Mungu wenye njia panda hawana tena kipawa cha Uangaji – na tena wanamiliki Amani ya uongo.

“Haya ndiyo maneno ya agano BWANA aliyomwagiza Mose kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya agano alilofanya nao huko Horebu. Hakikisheni kwamba hakuna mwanaume au mwanamke, ukoo au kabila miongoni mwenu leo ambalo moyo wake utamwacha BWANA Mungu wetu kwenda kuabudu miungu ya mataifa hayo, hakikisheni hakuna mzizi miongoni mwenu unaotoa sumu chungu ya namna hii. Wakati mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata kama nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.’’ Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyonyeshewa sawasawa na nchi kame”. (Kumbukumbu la Torati 29:1,18-19).

Kanisa kwa wakati huu limejaa wale wanao kubaliana na kutetea mambo ya giza. "kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. BWANA Mungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote. Ni BWANA Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye. Huyo nabii au mwota ndoto lazima auawe, kwa sababu amehubiri uasi dhidi ya BWANA Mungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, amejaribu kuwageuza kutoka njia ambayo BWANA Mungu wenu aliwaagiza mfuate. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu" (Kumbukumbu la Torati 13:3-5). Yeremia aliwaonya wale wanao tetea upotovu. Hanania alikuwa Muhubiri wa Amani na ufanisi wakati ambapo Mungu alikuwa na gadhabu na hasira ya hukumu. “Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, ‘Sikiliza Hanania! BWANA hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo. 16Kwa hiyo, hili ndilo asemalo BWANA: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya BWANA.’” (Yeremia 28:15-16). Manabii wa Ukweli wa Mungu waliwalaumu Wachungaji wa Israeli kwa Upofu huu wa ajabu mno. Yeremia alinguruma: “Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu na kulikanyaga shamba langu, watalifanya shamba langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.” (Yeremia 12:10). “Ole wa wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!’’ Asema BWANA”. (Yeremia 23:1). “Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapotosha na kuwasababisha kuzungukazungukajuu ya milima. Walitangatanga juu ya mlima na kilima na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia (Yeremia 50:6)

Shetani awanyemelea na kuwavamia Wachungaji! Akiweza kudanganya hata Mchungaji mmoja, kumpofusha kwa mambo fulani ya uasherati, atamuibia kipawa chake cha Uangaji na Mchungaji huyo ataishia akitetea maovu hapo mbele kwa madhabahu ya Bwana! Mimi Najua! Nilikuwa mmoja wa wale waliokuwa wanatetea maovu. Nilikuwa nawabembeleza wale waliovunja ndoa zao kwa sababau wakati huo ndoa yangu ilikuwa inakumbwa na misukosuko. Sikuweza kuwaonyesha watu wa Mungu upotovu wao kwa sababu nilikuwa na upotovu mimi mwenyewe kwa nafsi yangu. Mambo haya ya kimwili na kidunia, maubiri mepesi yatokana na wachungaji ambao wanaishi kwa dhambi. Kutokana na yale yalio jaa mioyono mwao wananena mafikiano na upotovu. Hawawezi kwa haki kuwaonesha watu wa Mungu uovu wao kwa sababu ya dhambi silizo fichika ndani ya mioyo yao wenyewe. Sikiliza neno la Mungu: “Nabii na kuhani wote si wacha Mungu, hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,’’ asema BWANA. (Yeremia 23:11). "...kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemu kutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.” (Yeremia 23:15). “Maono ya manabii wako yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, hawakuifunua dhambi yako katika kuzuilia kwenda kwako utumwani. Maneno waliyokupa yalikuwa ya uongo na ya kupotosha”. (Maombolezo 2:14). Walakini, Roho Mtakatifu sasa ainua Masalio, Wachungaji watakatifu na Watumishi waliobarikiwa na vipawa vya nguvu zaidi za Uangaji. Watawaongoza watu wa Mungu kwa HEKIMA mpya!

Hivi ndivyo vile huduma hii itakavyo kaa: “Lakini makuhani, ambao ni Walawi na wazao wa Sadoki wale ambao walitimiza wajibu wao kwa uaminifu katika patakatifu pangu wakati Waisraeli walipopotoka, watakaribia ili kutumika mbele zangu, itawapasa wasimame mbele zangu ili kutoa dhabihu za mafuta ya wanyama na damu, asema BWANA Mwenyezi. Wao peke yao ndio wenye ruhusa ya kuingia mahali patakatifu pangu, wao peke yao ndio watakaokaribia meza yangu ili kuhudumu mbele zangu na kufanya utumishi wangu.Watawafundisha watu wangu tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida na kuwaonyesha jinsi ya kupambanua kati ya vitu najisi na vitu safi”. (Ezekieli 44:15-16,23). Mungu Ainua Wachungaji Watakao Piga Tarumbeta, Kuwaonesha Watu Dhambi Zao, Na Kuwaita Watu Kurudi Katika Utakatifu Waliopokea Kutoka Kwa Yesu, Kulitii Neno La Mungu. “Piga kelele, usizuie. Paza sauti yako kama tarumbeta. Watangazieni watu wangu uasi wao na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao”. (Isaya 58:1). Wachungaji wa kweli wa Mungu wamekwisha sikia Mwito huu wa toba na wameanza kutii. Ninajazwa na furaha tele ninapo soma barua nyingi zinazofika ofisini mwetu kutoka kwa watumishi na wafanyikazi wakristo ambao wanatubu kwamba walikuwa wameanguka na kuwa baridi bila moto na upako wa Mungu. Sasa wana kiu maradufu ya utakatifu na kuoshwa kwa dhambi. Wanataka kuona Ufufuko wa Utakatifu katika Kanisa na Jamii zetu.

Uangaji wa kweli umuelekeza mtu kuona dhambi zake mwenyewe zilizo fichika moyoni mwake ili azikane na kuziepuka kwa Toba ya kweli. Uangaji inatuelekeza tuona ni umbali kiasi gani tumeteleza kutoka kwa usafi wa kiungu na basi kutusukuma kurudi tena kwa ile njia nyembamba. “Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu asemalo: “Msisikilize wanachowatabiria manabii, wanawajaza matumaini ya uongo. Wanasema maono kutoka katika akili zao wenyewe, hayatoki katika kinywa cha BWANA. Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi kwamba, BWANA asema: ‘Mtakuwa na amani.’ Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’ Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la BWANA ili kuona au kusikia neno lake? Ni nani aliyesikiliza na kusikia neno lake? Tazama, dhoruba ya BWANA itapasuka kwa ghadhabu, kisulisuli kitazunguka zunguka juu ya vichwa vya waovu. Hasira ya BWANA haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake. Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi. Mimi sikuwatuma manabii hawa, lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao, Mimi sikusema nao, lakini wametabiri. Lakini kama wangesimama barazani mwangu, wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu, nao wangewageuza kutoka katika njia zao mbaya na kutoka katika matendo yao maovu” (Yeremia 23:16-22).

(Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation - http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)

Download PDF