SISI NI WANA WA MUNGU KATIKA UZIMA AU KATIKA KIFO

David Wilkerson (1931-2011)

Kwa sababu Mungu anakupenda, atafanya kazi ya kukutakasa, lakini ni adhabu ya upendo kwa wale wanaotubu na kurudi kwake. Unaweza kuhisi mishale ya Mungu katika nafsi yako kwa sababu ya dhambi zako za zamani na za sasa, lakini ikiwa una moyo wa toba na unataka kuacha makosa, unaweza kuomba upendo wake wa kuadibu. Hutasikia ghadhabu yake kama watu wa mataifa mengine bali fimbo ya nidhamu yake, inayotumiwa na mkono wake wa upendo.

Unapojua umefika katika kiwango chako cha chini kabisa, ni wakati wa kumtafuta Bwana kwa uvunjaji, toba na imani.

Unapomlilia Mungu, anamimina nguvu zake ndani yako. “Siku ile nilipolia, ulinijibu, Ukanitia moyo kwa nguvu nafsini mwangu. Nijapokwenda katikati ya taabu, utanihuisha; utanyosha mkono wako juu ya ghadhabu ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa. Bwana atanikamilisha yale yanayonihusu; fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, ni za milele; usiziache kazi za mikono yako” (Zaburi 138:3, 7–8).

Moja ya mambo magumu sana kwa Wakristo kuyakubali ni mateso ya wenye haki. Kuna fundisho potofu linasema ukiwa katika makubaliano na Mungu, hutateseka kamwe. Inadai, “Muite tu Mungu, naye atakuja mbio na kutatua kila kitu mara moja.” Hii sio injili! Mashujaa wa imani walioorodheshwa katika Waebrania 11 wote walikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu, na waliteseka kwa dhihaka, mateso na vifo vikali (ona Waebrania 11:36–38). Paulo mwenyewe, ambaye alitembea kwa ukaribu na Mungu, alivunjikiwa meli, alipigwa mawe, akapigwa mijeledi, akaachwa akidhania kuwa amekufa, aliporwa, alifungwa gerezani na kuteswa. Alipata hasara ya vitu vyote.

Mungu anataka kupanda kitu ndani ya mioyo yetu kupitia majaribu yetu. Anataka tuweze kusema, “Bwana Yesu, ninaamini unatawala matukio ya maisha yangu. Ikiwa chochote kitanitokea, ni kwa sababu tu uliruhusu, na ninaamini kusudi lako la kulifanya. Nisaidie kuelewa somo unalotaka nijifunze kutokana nalo. Nikienenda katika haki na kuwa na furaha yako moyoni mwangu, kuishi kwangu na kufa kwangu kutakuletea utukufu. Nitasema; Yesu, ikiwa ninaishi au nikifa, mimi ni wako!”