UPWEKE UKO MAHALI POTE

Nicky Cruz

Tunahitaji kutofautisha kati ya kuwa mwenyewe, upweke na kutengwa. Kuwa mwenyewe, ni hali ya kujitenga na watu wengine. Wakati mwingine familia, marafiki na watu wengine kwa kutopatikanan mbele yetu, lakini tu kwa sababu sisi tuko wenyewe haimaanishi sisi tuko kwenye upweke. Tunachukua tu nyakati hizi kwa kuzingatia na kutambua kuwa maisha haiwezi kujazwa na watu daima.

Sasa, tunaweza kufikia mengi wakati sisi tuko wenyewe. Tunaweza kutumia muda tukiwa pamoja na Mungu na kuimarisha ushirika wetu naye. Mtunga-Zaburi Daudi aliandika hivi: "Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya, wokovu wangu hutoka kwake. Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, ngome yangu, sitatikisika sana" (Zaburi 62:1-2).

"Upweke ni uzoefu wa kawaida zaidi kwa sisi sote, lakini pia ni usioeleweka zaidi" (Ira J. Tanner, Upweke: Hofu ya Upendo). Upweke uko mahali pote; kila mtu hai ana anawupitia kwa kiwango fulani. Upekwe unaoona, haukusababishwa na mazingira yetu lakini ni hali ya akili. Ni hisia kwamba hakuna mtu na hakuna kitu kinachosikiliza njaa yetu ya kina kwa msaada na upendo.

Na kisha tuna kujitenga, nitendo la kujiondoa kwa makusudi kutoka kwa wengine kwa lengo la kuwa peke yake. Huu ndio wakati ambapo tunaweza kuwa vizuri kiroho na kujengwa tena kimawazo - wakati wa upya na ubunifu. Yesu mwenyewe alihitaji nyakati hizi za kutengwa ili awe na Baba yake wa mbinguni. "Naye alipokwisha kuaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake" (Mathayo 14:23).

Kitu kinachofanya Mkristo wa kisasa ni kutokana na ukosefu wa kujitenga. Tunakimbia hapa na huko kwenye matamasha, mikusanyiko, masomo ya Biblia, mikutano ya kupumzika, mikutano, na huduma za kila maelezo kwa kufikiri kwamba sisi "tunajaza kikombe chetu" – kila wakati nikushangaa kwa nini tunahisi tupu na, ndiyo, tukopeke yake, hata katikati umati wa watu. Lakini Yesu akasema, "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao ... nami nitawapumzisha" (Mathayo 11:28).

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza  ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka (Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco:Kimbiya , Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).