USHIRIKA WA KINA PAMOJA NA MUNGU
Henoko alifurahiya ushirika wa karibu na Bwana. Kwa kweli, ushirika wake na Mungu ulikuwa wa karibu sana hivi kwamba Bwana alimhamisha kwa utukufu muda mrefu kabla ya maisha yake hapa duniani kumalizika. "Kwa imani Henoko alichukuliwa ili asione mauti," na hakuonekana, kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua "; kwa maana kabla hajachukuliwa alikuwa na ushuhuda huu, ya kuwa alimpendeza Mungu” (Waebrania 11:5).