​UPENDO WA MUNGU NI MKUBWA ZAIDI

David Wilkerson (1931-2011)

Baba yetu wa mbinguni anataka tuwe na uhakika wa kudumu kuhusu upendo wake. Yesu aliweka tatizo la dhambi zetu huko Kalvari na hata ingawa sisi wakati mwingine tunashindwa, Roho Mtakatifu anatukumbusha daima huruma ya Baba. Tunapozingatia dhambi zetu, tunapoteza kila kitu ambacho Mungu anataka zaidi: "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana yeye anayekuja kwa Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko, na kwamba Yeye huwapa thawabu wale wamutafutao" (Waebrania 11:6).

Mungu ni mtowa thawabu, na ana hamu ya kutuosha kwa upendo wake wakati tunapotoshwa. Daudi ni mfano wa mtu aliyebarikiwa kwa wema wa Mungu ingawa alienda mbali katika dhambi. Unajua hadithi ya jinsi alivyoanguka katika uzinzi mkali na kisha alifanya mauaji ya kuepuka kupatikana nahatia. Daudi akawa mwaminifu, akifanya dhambi mbele ya baraka za Mungu na kuleta aibu kwa jina la Bwana. Hata hivyo, ingawa aliadhibiwa sana, Daudi alisamehewa na kurejeshwa kikamilifu.

Mungu alimtuma nabii Nathanaeli kumwambia Daudi juu ya dhambi yake kwa sababu ilikuwa ni tusi machoni pake. Lakini licha ya hilo, Mungu alitaka Daudi ajuwe kwamba amesamehewa. Unaona, Mungu alijua kwamba Daudi angevunjika na kusikitika juu ya dhambi yake; zaidi ya yote, Bwana alijua kwamba moyo wa Daudi hakuwa unazoweya uzinzi au mauaji. Badala yake, Daudi alishangazwa na dhambi, alizidiwa wakati wa muda wa udhaifu.

Vivyo hivyo, Mungu huona moyo wako. Bwana anajua kwamba wewe haukuamka asubuhi moja na ukamua, "Leo nitafanya uzinzi. Mimi nitapoteza hasira na kulipuka. "Hapana, wenye dhambi tu walio ngumu wanafanya hivyo. Wakristo wanashangaa na kuzidiwa na dhambi; Kwa kweli, mara nyingi adui huwa mafuriko yao wakati wao wanashugulika kuhusu kazi ya Mungu.

Wapendwa, Mungu alisha maliza kuhesabu machozi yenu hata kabla hamujayatowa. Amekusamehe kwa hatua ya kwanza ya imani na huzuni. "Wema wa Mungu unakuongoza kutubu" (Warumi 2:4). Upendo wake ni mkubwa zaidi kuliko dhambi zako zote!