ADUI KWA KILA UPANDE

David Wilkerson (1931-2011)

Shetani anawadanganya wengi katika Mwili wa Kristo, husababisha kukata tamaa na kuchanganyikiwa, na hawana changamoto katika nyumba ya Mungu. kwanini hivyo? Mahubiri mengi ya leo yanalenga kuzingatia mahitaji ya watu badala ya kuishi maisha ya ushindi ndani Kristo. Wahubiri hutoa jinsi ya mipango ya kupata tu na kukataa kabisa nafasi ya mbinguni tuliyopewa katika Kristo. Ukweli ni kwamba, ulimwengu huu umekuwa na shida, ambayo ina maana kwamba watu wa Mungu daima wanakabiliwa na adui ambae anawashambulia kutoka pande zote. Hali inabadilika, lakini shetani anaendelea kuwa vile vile.

Mwili wa Kristo unahitaji "uwamusho mkubwa" ... ufunuo na kuangaziwa. Paulo anasema hivi: "Kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ufunuo kwa kumjua yeye, macho ya ufahamu wenu apate mwanga; ili mujue tumaini la wito wake jinsi ulivyo, utajiri wa utukufu wa urithi wake ndani ya watakatifu jinsiulivyo, na ukuu mkubwa wa nguvu zake kwa sisi ambao tunaamini, kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake" ( Waefeso 1:17-19).

Paulo alikuwa anawaambia Waefeso, "Ninaomba kwamba Mungu atawapa ufunuo mpya na kufungua macho yenu kwa wito aliowapa. na ninaomba pia kuwapa uelewa mpya kuhusu urithi wenu, utajiri katika Kristo ambao ni wenu. Mungu anataka kuwatolea nguvu nyingi ndani yenu - nguvu sawa ile iliyokuwa ndani ya Yesu."

Kwa mujibu wa paulo, "Nguvu kuu [za Mungu] ambayo aliotenda ndani ya Kristo wakati alipomfufua kutoka kwa wafu na kumueka katika mkono wake wa kulia katika maeneo ya mbinguni" ni kama sawa "ukuu mkubwa wa nguvu Zake" kwamba sisi ambao tunaamini kuwa na uwezo ( ona waefeso 1:19-20).

Wapendwa, uhai wa nguvu hai sio uwigizaji au udanganyifu wa kidini. Ni utoaji unaowezekana kwetu kupitia msalaba wa Kristo, na "uwamusho" wako mwenyewe utakuja siku utapotazama maisha yako, na kumtazama yeye, na kulia sana, "Yesu, nakubali yale uliyonitendea na ninaomba nafasi yangu ndani yako."