AHADI YA YESU KWA AJILI YA UTOAJI WA KILA SIKU

Carter Conlon

Yesu mwenyewe alisisitiza umuhimu wa Neno wakati alitupa namna maalum ya kuomba: "Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, mapenzi yako atimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo mkate wa kila siku" (Mathayo 6:9-11). Juwa kwamba aliielezea kama "mkate wetu wa kila siku." Kuna utoaji wa kila siku ambao Yesu ameahidi kutupa.

Yesu alisema hivi hivi katika kitabu cha Yohana: "Mimi ndimi chakula cha uzima. Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mutu akile wala asife. Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu." (Yohana 6:48-51).

Yesu alikuwa akisema, "Mimi ni mkate! Mimi ni nguvu yako, maono yako, ukombozi wako, uhuru wako. Mimi ni mlinzi wako na mwongozo wako. Kila kitu unachohitaji kwa maisha na kimungu kinaweza kupatikana ndani yangu."

Kuzungumza kwa Biblia, nadhani mtu anaweza kusema kwamba wewe uko kitu unachokula! Ikiwa unachagua kwenda kwenye mlo kutoka kwa Biblia, utakuwa dhaifu, na hatimaye utaishia kuchanganyikiwa sana. Fikra zisizo sahihi zitaanza kukuongoza. Kisha, katika kukata tamaa kwako, utaanza kurejea televisheni na kusikiliza sauti ambazo hazizungumzi kweli. Watasimama mbele yako na kimsingi wanasema, "Angalia! Hii ndio maisha ya Kikristo inavyoonekana. Njoo, unifuate!"

Ikiwa hausomi Neno la Mungu - hutakula huu Mkate wa Uhai – utaishia kwa kupotoshwa mwishoni mwa siku zako.

Carter Conlon alijiunga na  jopo la wachungaji wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji  muanzilishi, David Wilkerson, na alichaguliwa  kuwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.