AMANI TELE YA KRISTO

David Wilkerson (1931-2011)

"Amani nawaachieni; amani yangu nawapa" (Yohana 14:27). Neno hili la ajabu kutoka kwa Yesu liliwashangaza wanafunzi. Kwa macho yao, ilikuwa ahadi ya karibu isiyowezekana: Amani ya Kristo ilikuwa amani yao. Wanaume kumi na wawili walishangaa kwa amani waliyoiona kutoka kwa Yesu kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Mwalimu wao alikuwa daima na utulivu, asie kuwa na hofu kamwe, kamwe kuharibiwa na hali yoyote. na sasa Yesu alikuwa akiwaahidi Amani hio hio!

Kisha Yesu aliongeza, "Sivyo kama ulimwengu utoavyo" (mstari huo). Hii haikuwa amani ya muda, ao amani ambao inatokana kwa kununuwa vitu vyenye samani kubawa . Apana, hii ilikuwa ni amani kutoka kwa Kristo mwenyewe, amani inayozidi ufahamu wowote wa kibinadamu.

Muda wa karama hii ya amani ulikuwa muhimu sana kwa wanafunzi kwa sababu walikuwa kwenye kizingiti cha majaribio makubwa zaidi waliopitia. Kristo alikuwa karibu kuwaacha, na habari ya kuondoka kwake kwa karibu ilikuja kama mshtuko mkubwa. Walikuwa wanatazamia siku ambayo bwana angeanzisha ufalme wake duniani na kuwafanya wawe watawala wote. Sasa walipaswa kukabiliana na ukweli kwamba alikuwa karibu kutiwa katika mikononi ya wanadamu na kuuawa.

"Nitafufuliwa tena," Mwalimu aliwahakikishia, "Na Roho Mtakatifu atawaongoza kupitia yale mutakaokutana na." Wakati huu, yote ambayo wanafunzi yalikuwa ni ahadi kutoka kwa Kristo kuhusu amani yake.

Kazi ya Roho Mtakatifu imekuwa daima nikufunuwa Kristo kwa watu wake. Katika Yohana 16:14, anasema, kwa kifupi, "Roho Mtakatifu atawaambia ninyi kuhusu mimi na njia zangu." Kwa kifupi, amani yake inatujia kupitia Roho Mtakatifu kwa kutufunulia Kristo.

Wakati ulipopokea Kristo, ulipokea kipimo cha Roho yake na kazi ya Roho inaendelea ndani yako hadi leo.