ANGALIA MFALME WETU MWENYE UTUKUFU
Inaonekana dunia nzima inatetemeka hivi sasa juu ya matukio ya sasa. karibu kila siku tunaamka kwa maendeleo mengine yanayochochea msingi wetu, inaonekana hivo. Katika mwaka uliopita dunia imekuwa na mafuriko ya kuvunja rekodi, moto unaoharibu ambao unaangamiza miji yote, vimbunga, tetemeko la ardhi. na kisha tuna kasi ya kupoteza maadili ya jamii yetu.
Kwa kwa mambo ya kidunia, inaonekana kama hakuna mtu anayehusika. Wasioamini wanajiambia kwamba hakuna jibu linabakiya, kwa kuwa kila kitu kinazunguka katika machafuko. Tunajua kwamba hakuna sababu ya hofu, kwa sababu biblia inatukumbusha mara kwa mara kwamba bwana ana kila kitu kilicho chini ya udhibiti wake. Hakuna kitu kimoja kinachofanyika ulimwenguni bila ujuzi wake na utawala.
Mtunga-Zaburi anaandika, "Maana ufalme ni wa Bwana, naye ndiye anatawalaye mataifa" (Zaburi 22:28). Vivyo hivyo, nabii isaya hutangazia ulimwengu, "Njoni, ninyi mataifa, msikie; sikirizeni enyi kabila za watu! Dunia na isikie, na vyote vilivyomo" (Isaya 34:1). anasema, "Sikieni, mataifa, na muinuwe masikio yenu. Ninataka kukuambia jambo muhimu kuhusu muumba wa dunia."
Isaya anasema kwamba wakati ghadhabu ya Mungu itakapopandishwa dhidi ya mataifa na majeshi yao, ni Bwana mwenyewe ndie ambaye atawokoa. "Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kama mavumbi madogo juu ya mizani ... Mataifa yote huwa kama sikitu mbele zake; huhesabiwa kwake, na wao huhesabiwakwake kuwa duniya sikitu cha maana ... Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi" (Isaya 40:15, 17, 22).
Isaya anawashauri watu wa Mungu, ambao wanasumbuliwa na wasiwasi na matukio ya ulimwengu, "Angalieni juu, mbingu za utukufu. Tazama milioni ya nyota na Mungu wako ndie ameziumba na aitaye kila mmoja. Je, wewe sio mwenye thamani zaidi kuliko hizo? Basi usiogope!
Unawezaje kuwa na wasiwasi kuhusu mgogoro wako? Neno lake ni ahadi yenye ukamilifu na matumaini, hivyo likumbatieni kwake bila kujali kitu kingine.