ATHARI YA WATUMISHI WAAMINIFU

Gary Wilkerson

Yohana Mbatizaji aliitwa kutayarisha njia ya Yesu. Hakushika mtu binafsi na kumwambia kama alikuwa anakwenda kusimamisha kufanya jambo moja na kuanza kufanya jambo lingine. Hapana, alitangaza kwamba Yesu alikuwa amekuja kwa ajili ya watu waliojitolea kwa sababu ya Kristo, watu ambao wangejitoa kwa uhakika kabisa.

Bwana alimwambia Zakaria kuhusu Yohana, "Naye atatangulia mbele za Bwana, kwa roho na nguvu ya Eliya, ili kugeuza miyo ya baba iwaelekee watoto na kuwatilia waasi akili za wenye haki – na kutayarisha watu waliotayari kwa ajili ya Bwana" (Luka 1:17, NIV).

Yesu alikuwa amekuja kwa watu wariojitayarisha - sio jengo au mpango au hata kundi. Mungu anataka mwili wa waumini ambao wamejitolea kwa kweli katika vitu vinavyotuleta pamoja - watumishi waaminifu ambao wamejazwa na Roho Mtakatifu na nguvu ya Eliya.

Tunasoma tena kuhusu Eliya katika Yakobo: "Eliya alikuwa mtu mwenye asili kama yetu, na aliomba kwa bidii ili mvua isiweze, na kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita hakuwa mvua duniani. Kisha akaomba tena, mbinguni ikatoa mvua, na nchi ikazaza matunda yake" (Yakobo 5: 17-18).

Neno la Mungu linasema kwamba Eliya alikuwa mtu kama sisi, lakini alifanya vitu ambavyo vilikuwa nje ya kawaida. Lakini tunasomea zaidi katika Yakobo: "Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejesha; jueni ya kuwa yeye amrejeshaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi." (5:19-20).

Kuwa na imani ya kusimamisha mvua au kuomba mvua nchini, kama Eliya alivyofanya, ni nguvu, kwa kweli. Lakini kuokoa mtu kutoka kifo ni ajabu sana na, kulingana na Yakobo, Yesu ametoa yote, ndio wewe na mimi, ambao tunakwenda pamoja naye kwa nguvu na mamlaka ya kufanya hivyo tu.