BEI YA MAMLAKA YA KIROHO

David Wilkerson (1931-2011)

Kuwa mtumishi wa tabia nzuri ambaye huenda katika mamlaka ya Mungu, inatuhitaji kusimama uso kwa uso na dhamiri yetu machoni pa Baba yetu. Tunaposimama mbele za Bwana, tunaingizwa kwa magoti yetu kwa unyenyekevu mbele ya uwepo wake mtakatifu.

Mtume Paulo anaelezea namna ya mtumishi ambaye mamlaka amepewa mamulaka hayo: "[Ameacha] mambo yaliyofichwa ya aibu, wala kutoendana kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu kwa udanganyifu" (2 Wakorintho 4:2).

Mtumishi huyo amefungwa na Yesu na amefungua moyo wake kwa matendo ya Roho Mtakatifu. Kwa mujibu wa Paulo, sala ya mara kwa mara ya mtumishi huyu ni: "Bwana, nionyeshe nia zangu za dhambi, na kutamani kwangu kusiyo kuzuri, kutoku na uaminifu wowote au udanganyifu wowote, na tabia yoyote ya siri, ya udanganyifu katika moyo wangu."

Naamini waumini wote wanataka kutembea katika mamlaka ya kiroho lakini ni muhimu kutambua kwamba kuna bei ya kulipwa kwa mamlaka hiyo. Swali moja nzuri kujiuliza ni: "Je! Nimekubali kiti cha chini sana ndani ya nyumba? Je, ninafurahi kukaa mbali na meza ya mbele?" Ni mtihani rahisi, lakini inawezakana kufungua mambo muhimu katika roho yako.

Katika Luka 14, tunaona kwamba Yesu alialikwa na mu Farisayo mkuu kwa "kula mkate" nyumbani kwake pamoja na Mafarisayo wengine. Mstari wa 7 unasema kwamba Yesu aliwaona wakichagua viti vyema kwa sababu ya kiburi chao na haja ya kuonekana na kutambuliwa. Bwana akaketi kula na kisha akawapa akawambia neno viongozi wa kidini wenye mamulaka makubwa katika Israel kwa kuwakemea: "Unapoalikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma kabisa, ili ijapo yule aliyekualika akuambie, rafiki yangu njoo huku mbele zaidi" (Luka 14:10).

Tunapaswa kujitahidi "kwenda juu" katika mahali pa heshima ya haki, mahali pa mamlaka ya kweli ya kiroho. Mungu anahitaji kila mmoja wetu katika siku hizi za mwisho na anataka tukaribie. Kwa maana kubwa sana, naamini kazi ya kumkaribia Yesu ni kwa sisi sote. Kwa kufanya hivyo, Mungu atawumwagia uaminifu wake kwa upako wa kiroho.