BILA KUJALI UNACHOFIKIRI
Tunapokubali utiwaji wa Roho Mtakatifu, tunatimiza agizo hili: "Amin, Amin nwambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba" (Yohana 14:12). Dunia nzima inahitaji uponyaji wake, utakaso, nguvu za kuokoa, na kwamba hutokea tu kwa dhabihu yake kamilifu: "Kwa kuwa mimi naenda kwa Baba."
Usiwe na shaka kwa nafasi yoyote ambayo Yesu anakuletea. Kitu muhimu kwa hili, ni kuamini kwamba yeye anafanya kazi daima. Wanafunzi walipomwomba Yesu kuwapa imani, jibu lake linatuambia kila kitu: "Nawaambieni kwa kweli, ikiwa mngelikuwa na imani hata kidogo kama mbegu ya haradali, mngeweza kusema kwa mlima huu, 'Ondoka hapa uende kule,' nao ungeondoka. Wala halitakuwepo neon lisilowezekana kwamwe" (Mathayo 17:20, NLT).
Licha ya zawadi za ajabu kutoka kwa Kristo kwa ajili yetu, baadhi yetu tunaamini kwamba hatukustahili kuiwakilisha injili yake. Kwa kweli hiyo inapuza asili ya injili. Tunakuwa wawakilishi wake watakatifu sio kwa uwezo wetu bali kwa kazi ya Mungu ndani yetu: "Yeye aliyeanza kazi njema ndani ya mioyoni mwenu ataimaliza hata ataifanya siku ya Kristo Yesu" (Wafilipi 1:6).
Petro alikuwa labda Mkristo wa kwanza kufundishwa ukweli huu wenye nguvu. Katika Matendo 10 wakati alipokuwa akiishi Yafa kwa mtengenezaji wa ngozi aitwaye Simoni, Petro alikuwa na maono wakati wa maombi ambayo alifanya kuenea kwa injili ya Kristo mpaka leo. Yeye alishangazwa na maono, lakini aliitii mwongozo wa Mungu na mlango wa uponyaji, na nguvu ya kuokoa ya Mungu ilifunguliwa kwa ulimwengu (soma akaunti katika Matendo 10:9-48).
Haijalishi ni nini ambacho leo unafikili, nakuhimiza kukubali utakatifu wake na kupokea upako wake utimize kazi aliyokuandalia. Atafungua kila mlango na utamwona yeye akifanya maajabu yasiyotarajiwa.