BWANA AKUBARIKI NA KUKULINDA

David Wilkerson (1931-2011)

Ninaomba kwa bidii juu ya jumbe hizi, na wakati nikiomba kuhusu kile ambacho Bwana angenitaka niandike katika huu, Roho Mtakatifu alinong’ona kwa uwazi, “Watie moyo watu wa Mungu. Waambie jinsi Bwana anavyowapenda na jinsi anavyowafurahia watoto wake.”

Ninaamini hili ni neno maalum kwa wengi wanaosoma ujumbe huu. Unahitaji kusikia ndani kabisa, katika saa hii hii, kwamba Bwana atakulinda na kwamba anapendezwa nawe katika saa yako ya kujaribiwa. Hapa kuna maandishi ninaamini unahitaji kupokea kama neno la kibinafsi kutoka kwake hivi sasa:

“Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, wala usichukie kurudiwa kwake; kwa maana Bwana ampendaye humrudi, kama vile baba mwana ambaye amependezwa naye” (Mithali 3:11-12).

“Ee Bwana, nimekutumaini wewe; nisione haya kamwe; uniokoe kwa haki yako.... Mikononi mwako naiweka roho yangu; umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli” (Zaburi 31:1, 5).

“Nimewachukia wale wanaozingatia sanamu zisizofaa; lakini ninamtumaini Bwana. Nitashangilia na kuzifurahia fadhili zako, kwa maana umeyatafakari taabu yangu; umeijua nafsi yangu katika taabu, wala hukunitia mkononi mwa adui; umeiweka miguu yangu mahali palipo pana” (Zaburi 31:6-8).

“Umehesabu kutanga-tanga kwangu; uyatie machozi yangu katika chupa yako; hayamo katika kitabu chako? Nitakapokulilia, ndipo adui zangu watarudi nyuma; Najua hili, kwa kuwa Mungu yu upande wangu” (Zaburi 56:8-9).

Hata kama unayopitia sasa hivi ni nidhamu ya upendo, kumbuka ni ishara ya hakika Baba yako anakupenda na anafurahishwa nawe. Ikiwa utapokea neno hili kwamba anakupenda sana na anafurahi juu yako, utajua mambo yote yanakwenda kwa manufaa yako na kwamba hatua zako zinaamriwa na yeye.

Tafadhali pigia mstari sehemu ya maandiko ambayo Roho anashuhudia ni yako. Amini! Mungu ameituma kwako leo.

 
Child smiling - More Hope in 2025

You Can Bring Real Hope

 

In 2024 millions have been ministered to online. Thousands of disciples have been made. Hundreds of churches have been planted. Dozens of communities have been transformed both spiritually and physically. This is the power of the gospel at work through your financial partnership with World Challenge.